Isaya Mlango 3 Isaiah

Isaya 3:1 Isaiah 3:1

Kwa maana, tazama, Bwana, Bwana wa majeshi, awaondolea Yerusalemu na Yuda egemeo na tegemeo; tegemeo lote la chakula na tegemeo lote la maji;

Isaya 3:2 Isaiah 3:2

mtu hodari na mtu wa vita; mwamuzi na nabii; mpiga ramli na mzee;

Isaya 3:3 Isaiah 3:3

jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye mstadi, na mganga ajuaye uganga sana.

Isaya 3:4 Isaiah 3:4

Nami nitawapa watoto kuwamiliki, na watoto wachanga kuwatawala.

Isaya 3:5 Isaiah 3:5

Nao watu wataonewa, kila mtu na mwenziwe, na kila mtu na jirani yake; mtoto atajivuna mbele ya mzee, na mtu mnyonge mbele ya mtu mwenye heshima.

Isaya 3:6 Isaiah 3:6

Mtu atakapomshika ndugu yake ndani ya nyumba ya baba yake, akisema, Wewe una nguo, ututawale wewe; na mahali hapa palipobomoka pawe chini ya mkono wako;

Isaya 3:7 Isaiah 3:7

basi, siku ile atainua sauti yake, akisema, Mimi sitakuwa mponya watu; kwa maana ndani ya nyumba yangu hamna chakula wala mavazi; wala hamtanifanya kuwa mtawala juu ya watu hawa.

Isaya 3:8 Isaiah 3:8

Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha Bwana, hata wayachukize macho ya utukufu wake.

Isaya 3:9 Isaiah 3:9

Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu.

Isaya 3:10 Isaiah 3:10

Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao

Isaya 3:11 Isaiah 3:11

Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa ijara ya mikono yake.

Isaya 3:12 Isaiah 3:12

Katika habari za watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.

Isaya 3:13 Isaiah 3:13

Bwana asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu.

Isaya 3:14 Isaiah 3:14

Bwana ataingia katika kuwahukumu wazee wa watu wake na wakuu wao; Ninyi ndinyi mliokula shamba la mizabibu; vitu mlivyowateka maskini vi ndani ya nyumba zenu.

Isaya 3:15 Isaiah 3:15

Ni nini maana yake, ninyi kuwaonea watu wangu, na kuseta nyuso za maskini? Asema Bwana, Bwana wa majeshi.

Isaya 3:16 Isaiah 3:16

Bwana akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;

Isaya 3:17 Isaiah 3:17

Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na Bwana ataifunua aibu yao.

Isaya 3:18 Isaiah 3:18

Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;

Isaya 3:19 Isaiah 3:19

na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;

Isaya 3:20 Isaiah 3:20

na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu;

Isaya 3:21 Isaiah 3:21

na pete, na azama,

Isaya 3:22 Isaiah 3:22

na mavazi ya sikukuu, na debwani; na shali, na vifuko;

Isaya 3:23 Isaiah 3:23

na vioo vidogo, na kitani nzuri, na vilemba, na utaji.

Isaya 3:24 Isaiah 3:24

Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.

Isaya 3:25 Isaiah 3:25

Watu wako waume wataanguka kwa upanga, na mashujaa wako vitani.

Isaya 3:26 Isaiah 3:26

Na malango yake yatalia na kuomboleza, naye atakuwa ukiwa, atakaa chini.