Isaya Mlango 32 Isaiah

Isaya 32:1 Isaiah 32:1

Tazama, mfalme atamiliki kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu.

Isaya 32:2 Isaiah 32:2

Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu.

Isaya 32:3 Isaiah 32:3

Tena macho yao waonao hayatakuwa na kiwi, na masikio yao wasikiao yatasikiliza.

Isaya 32:4 Isaiah 32:4

Tena moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu maarifa, na ndimi zao wenye kigugumizi zitakuwa tayari kunena sawasawa.

Isaya 32:5 Isaiah 32:5

Mpumbavu hataitwa tena mwungwana, wala ayari hatasemwa kwamba ni karimu.

Isaya 32:6 Isaiah 32:6

Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya Bwana, ili kuziacha nafsi za watu wenye njaa hazina kitu, na kukikomesha kinywaji chake mwenye kiu.

Isaya 32:7 Isaiah 32:7

Tena vyombo vyake ayari ni vibaya; hutunga hila mbaya, ili kuwaangamiza wanyonge kwa maneno ya uongo, mtu mhitaji ajaposema maneno yenye haki.

Isaya 32:8 Isaiah 32:8

Bali mwungwana huwaza mambo ya kiungwana, naye hushika sana mambo ya kiungwana.

Isaya 32:9 Isaiah 32:9

Inukeni, enyi wanawake wenye raha, isikieni sauti yangu; enyi binti za watu msiokuwa na uangalifu, tegeni masikio yenu msikie matamko yangu.

Isaya 32:10 Isaiah 32:10

Maana mtataabishwa siku kadha wa kadha zaidi ya mwaka, enyi wanawake mliojikinai; kwa sababu mavuno ya mizabibu yatakoma, wakati wa kuvuna vitu vya mashamba hautakuja.

Isaya 32:11 Isaiah 32:11

Tetemekeni, enyi wanawake wenye raha; taabikeni, enyi msiokuwa na uangalifu; jivueni, jivueni nguo zenu kabisa, jivikeni viuno nguo za magunia.

Isaya 32:12 Isaiah 32:12

Watajipiga vifua kwa ajili ya mashamba mazuri, kwa ajili ya mzabibu uliozaa sana.

Isaya 32:13 Isaiah 32:13

Juu ya nchi ya watu wangu itamea michongoma na mibigili; naam, juu ya nyumba za furaha katika mji ulio na shangwe;

Isaya 32:14 Isaiah 32:14

maana jumba la mfalme litaachwa; mji uliokuwa na watu wengi utakuwa hauna mtu; kilima na mnara utakuwa makao ya wanyama milele, furaha ya punda-mwitu, malisho ya makundi ya kondoo;

Isaya 32:15 Isaiah 32:15

hata roho itakapomwagwa juu yetu kutoka juu; hata jangwa litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa msitu.

Isaya 32:16 Isaiah 32:16

Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana.

Isaya 32:17 Isaiah 32:17

Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.

Isaya 32:18 Isaiah 32:18

Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu.

Isaya 32:19 Isaiah 32:19

Lakini mvua ya mawe itakunya, wakati wa kuangushwa miti ya msituni; na huo mji utadhilika.

Isaya 32:20 Isaiah 32:20

Heri ninyi mpandao mbegu kando ya maji yote, na kuiacha miguu ya ng'ombe na punda waende ko kote.