Isaya Mlango 17 Isaiah

Isaya 17:1 Isaiah 17:1

Ufunuo juu ya Dameski. Tazama, Dameski umeondolewa usiwe mji, nao utakuwa chungu ya magofu.

Isaya 17:2 Isaiah 17:2

Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu.

Isaya 17:3 Isaiah 17:3

Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema Bwana wa majeshi.

Isaya 17:4 Isaiah 17:4

Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua-pungua, na kunona kwa mwili wake kutakonda.

Isaya 17:5 Isaiah 17:5

Tena itakuwa kama hapo avunaye ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.

Isaya 17:6 Isaiah 17:6

Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema Bwana, Mungu wa Israeli.

Isaya 17:7 Isaiah 17:7

Katika siku hiyo mwanadamu atamwangalia Muumba wake, na macho yake yatamtazama Mtakatifu wa Israeli.

Isaya 17:8 Isaiah 17:8

Wala hataziangalia madhabahu, kazi ya mikono yake; wala hatavitazama vilivyofanyika kwa vidole vyake, maashera na sanamu za jua.

Isaya 17:9 Isaiah 17:9

Katika siku hiyo miji yake yenye maboma itakuwa kama mahali palipoachwa ndani ya mwitu, na juu ya kilele cha mlima, palipoachwa mbele ya wana wa Israeli; napo patakuwa ganjo.

Isaya 17:10 Isaiah 17:10

Maana umemsahau Mungu wa wokovu wako, wala hukuukumbuka mwamba wa ngome yako; kwa sababu hiyo ulipanda mashamba yapendezayo, na kutia ndani yake mizabibu migeni.

Isaya 17:11 Isaiah 17:11

Katika siku ile ulipopanda, ulifanya kitalu, na wakati wa asubuhi ulizimeesha mbegu zako, lakini mavuno yatatoweka siku ya huzuni, na ya sikitiko la moyo lifishalo.

Isaya 17:12 Isaiah 17:12

Aha! Uvumi wa watu wengi! Wanavuma kama uvumi wa bahari; Aha! Ngurumo ya mataifa! Wananguruma kama ngurumo ya maji mengi;

Isaya 17:13 Isaiah 17:13

Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.

Isaya 17:14 Isaiah 17:14

Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu; Na kabla ya mapambazuko hawako; Hilo ndilo fungu lao watutekao, Na ajali yao wanaotunyang'anya mali zetu.