Isaya Mlango 24 Isaiah

Isaya 24:1 Isaiah 24:1

Tazama, Bwana ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake.

Isaya 24:2 Isaiah 24:2

Na itakuwa kama ilivyo hali ya watu, ndivyo itakavyokuwa hali ya kuhani; kama ilivyo hali ya mtumwa, ndivyo itakavyokuwa hali ya bwana wake; kama ilivyo hali ya mjakazi, ndivyo itakavyokuwa hali ya bibi yake; kama ilivyo hali yake anunuaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake auzaye; kama ilivyo hali yake akopeshaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake akopaye; kama ilivyo hali yake atwaaye faida, ndivyo itakavyokuwa hali yake ampaye faida.

Isaya 24:3 Isaiah 24:3

Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana Bwana amenena neno hilo.

Isaya 24:4 Isaiah 24:4

Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika.

Isaya 24:5 Isaiah 24:5

Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.

Isaya 24:6 Isaiah 24:6

Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.

Isaya 24:7 Isaiah 24:7

Divai mpya inaomboleza, mzabibu umedhoofika, watu wote waliochangamka moyo wanaugua.

Isaya 24:8 Isaiah 24:8

Sauti ya furaha ya matoazi inakoma; kelele yao wafurahio imekwisha; furaha ya kinubi inakoma.

Isaya 24:9 Isaiah 24:9

Hawatakunywa divai pamoja na nyimbo; kileo kitakuwa uchungu kwao wakinywao.

Isaya 24:10 Isaiah 24:10

Mji wa machafuko umebomolewa; kila nyumba imefungwa, asipate kuingia mtu awaye yote.

Isaya 24:11 Isaiah 24:11

Pana kilio katika njia kuu kwa sababu ya divai; furaha yote imetiwa giza, na changamko la nchi limetoweka.

Isaya 24:12 Isaiah 24:12

Ndani ya mji umebaki ukiwa, na lango lake limepigwa kwa uharibifu.

Isaya 24:13 Isaiah 24:13

Maana katikati ya dunia, katikati ya mataifa, itakuwa hivi; kama wakati utikiswapo mzeituni, kama wakati waokotapo zabibu baada ya mavuno yake.

Isaya 24:14 Isaiah 24:14

Hawa watainua sauti zao, watapiga kelele; kwa sababu ya utukufu wa Bwana watapiga kelele toka baharini.

Isaya 24:15 Isaiah 24:15

Basi, mtukuzeni Bwana katika mashariki, litukuzeni jina la Bwana, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari.

Isaya 24:16 Isaiah 24:16

Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. Ndipo niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu! Watenda hila wametenda hila, naam, watendao hila wametenda hila sana.

Isaya 24:17 Isaiah 24:17

Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.

Isaya 24:18 Isaiah 24:18

Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika.

Isaya 24:19 Isaiah 24:19

Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana.

Isaya 24:20 Isaiah 24:20

Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.

Isaya 24:21 Isaiah 24:21

Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana ataliadhibu jeshi la mahali palipo juu katika mahali palipo juu, na wafalme wa dunia katika dunia;

Isaya 24:22 Isaiah 24:22

nao watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza; na baada ya muda wa siku nyingi watajiliwa.

Isaya 24:23 Isaiah 24:23

Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa Bwana wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.