Isaya Mlango 15 Isaiah

Isaya 15:1 Isaiah 15:1

Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.

Isaya 15:2 Isaiah 15:2

Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.

Isaya 15:3 Isaiah 15:3

Wanajivika nguo za magunia katika njia kuu zao; juu ya dari zao, na katika mitaa yao, kila mtu analia, anamwaga machozi.

Isaya 15:4 Isaiah 15:4

Heshboni analia na Eleale; mpaka Yahasa sauti ya kulia kwao inasikiwa; hata watu wa Moabu waliovaa silaha wanapiga kelele sana kwa sababu hiyo; nafsi yake inatetemeka ndani yake.

Isaya 15:5 Isaiah 15:5

Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanapaliza sauti ya kukata tamaa.

Isaya 15:6 Isaiah 15:6

Kwa maana maji ya Nimrimu yamekuwa mahali palipoharibika, kwa kuwa majani yamekauka, miche imenyauka, majani mabichi yamekoma.

Isaya 15:7 Isaiah 15:7

Kwa hiyo vitu walivyojipatia tele, na akiba yao, wanavichukua hata kijito cha mierebi.

Isaya 15:8 Isaiah 15:8

Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu.

Isaya 15:9 Isaiah 15:9

Maana maji ya Dimoni yamejaa damu; maana ninaweka tayari msiba mpya juu ya Dimoni, simba juu ya watu wa Moabu waliokimbia, na juu ya mabaki yao.