Isaya Mlango 28 Isaiah

Isaya 28:1 Isaiah 28:1

Ole wa taji ya kiburi ya walevi wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la hao walioshindwa na divai!

Isaya 28:2 Isaiah 28:2

Tazama, Bwana ana mmoja aliye hodari, mwenye nguvu; kama dhoruba ya mvua ya mawe, tufani iharibuyo, kama dhoruba ya maji mengi yafurikayo, ndivyo atakavyotupa chini kwa mkono.

Isaya 28:3 Isaiah 28:3

Taji ya kiburi ya walevi wa Efraimu itakanyagwa kwa miguu;

Isaya 28:4 Isaiah 28:4

na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, litakuwa kama tini iliyotangulia kuiva kabla ya wakati wa hari, ambayo, aionapo yeye aiangaliaye, huila mara anapoishika mkononi mwake.

Isaya 28:5 Isaiah 28:5

Katika siku ile Bwana wa majeshi atakuwa ni taji ya fahari, na kilemba cha uzuri, kwa mabaki ya watu wake.

Isaya 28:6 Isaiah 28:6

Naye atakuwa roho ya hukumu kwake yeye aketiye ili ahukumu; naye atakuwa nguvu kwao wageuzao nyuma vita langoni.

Isaya 28:7 Isaiah 28:7

Lakini hawa nao wamekosa kwa divai, wamepotea kwa kileo; kuhani na nabii wamekosa kwa kileo, wamemezwa kwa divai, wamepotea kwa kileo; hukosa katika maono, hujikwaa katika hukumu.

Isaya 28:8 Isaiah 28:8

Maana meza zote zimejaa matapiko na uchafu, hapana mahali palipo safi.

Isaya 28:9 Isaiah 28:9

Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini?

Isaya 28:10 Isaiah 28:10

Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo.

Isaya 28:11 Isaiah 28:11

La, bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa;

Isaya 28:12 Isaiah 28:12

ambao aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yeye aliyechoka; huku ndiko kuburudika; lakini hawakutaka kusikia.

Isaya 28:13 Isaiah 28:13

Kwa sababu hiyo neno la Bwana kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa.

Isaya 28:14 Isaiah 28:14

Basi, lisikieni neno la Bwana, enyi watu wenye dharau, mnaowatawala watu hawa walio ndani ya Yerusalemu.

Isaya 28:15 Isaiah 28:15

Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;

Isaya 28:16 Isaiah 28:16

kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.

Isaya 28:17 Isaiah 28:17

Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na mvua ya mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha mahali pa kujisitiri.

Isaya 28:18 Isaiah 28:18

Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo.

Isaya 28:19 Isaiah 28:19

Kila wakati litakapopita litawachukueni. Maana litapita asubuhi baada ya asubuhi, wakati wa mchana na wakati wa usiku; na kuifahamu habari ile kutakuwa kitisho tu.

Isaya 28:20 Isaiah 28:20

Maana kitanda kile ni kifupi asiweze mtu kujinyosha juu yake, na nguo ile ya kujifunika ni nyembamba asipate mtu kujizingisha.

Isaya 28:21 Isaiah 28:21

Maana Bwana ataondoka kama vile katika mlima Perasimu, ataghadhibika kama vile katika bonde la Gibeoni; apate kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu; na kulitimiza tendo lake, tendo lake la ajabu.

Isaya 28:22 Isaiah 28:22

Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, Bwana wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.

Isaya 28:23 Isaiah 28:23

Tegeni masikio, sikieni sauti yangu, sikilizeni mkasikie neno langu.

Isaya 28:24 Isaiah 28:24

Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima madongoa ya nchi yake, na kuyavunja?

Isaya 28:25 Isaiah 28:25

Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huko na huko kunde, na kutupa-tupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake?

Isaya 28:26 Isaiah 28:26

Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha.

Isaya 28:27 Isaiah 28:27

Kwa maana kunde zile hazipurwi kwa chombo kikali, wala gurudumu la gari halipitishwi huko na huko juu ya jira ile, bali kunde zile hupurwa kwa fimbo, na jira ile kwa ufito.

Isaya 28:28 Isaiah 28:28

Ngano ya mkate husagwa; kwa maana haipuri siku zote bila kukoma; na ingawa gurudumu la gari lake na farasi wake huitawanya ngano ile, haisagi.

Isaya 28:29 Isaiah 28:29

Hayo nayo yatoka kwa Bwana wa majeshi, mwenye shauri la ajabu, apitaye wote kwa hekima yake.