Isaya Mlango 8 Isaiah

Isaya 8:1 Isaiah 8:1

Bwana akaniambia, Ujipatie ubao mkubwa ukaandike juu yake kwa kalamu ya binadamu, Kwa Maher-shalal-hash-bazi;

Isaya 8:2 Isaiah 8:2

nami nitajipatia mashahidi waaminifu ili kuandika habari, yaani, Uria, kuhani, na Zekaria, mwana wa Yeberekia.

Isaya 8:3 Isaiah 8:3

Nami nikamwendea huyo nabii mke, naye akapata mimba, akazaa mtoto mwanamume. Kisha Bwana akaniambia, Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi.

Isaya 8:4 Isaiah 8:4

Kwa maana kabla mtoto huyo hajapata kujua kusema, Baba yangu, na Mama yangu, hazina za Dameski na mateka ya Samaria yatachukuliwa mbele ya mfalme wa Ashuru.

Isaya 8:5 Isaiah 8:5

Kisha Bwana akasema nami mara ya pili, akaniambia,

Isaya 8:6 Isaiah 8:6

Kwa sababu watu hawa wameyakataa maji ya Shiloa yapitayo polepole, na kufurahi kwa ajili ya Resini na huyo mwana wa Remalia,

Isaya 8:7 Isaiah 8:7

basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo Mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote, atafurika juu ya kingo zake zote;

Isaya 8:8 Isaiah 8:8

naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.

Isaya 8:9 Isaiah 8:9

Fanyeni ghasia, enyi kabila za watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande.

Isaya 8:10 Isaiah 8:10

Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.

Isaya 8:11 Isaiah 8:11

Maana Bwana aliniambia hivi, kwa mkono hodari, akanifundisha nisiende katika njia ya watu hawa, akisema,

Isaya 8:12 Isaiah 8:12

Msiseme, Ni fitina, katika habari za mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni fitina; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope.

Isaya 8:13 Isaiah 8:13

Bwana wa majeshi ndiye mtakayemtakasa; na awe yeye hofu yenu, na awe yeye utisho wenu.

Isaya 8:14 Isaiah 8:14

Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.

Isaya 8:15 Isaiah 8:15

Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.

Isaya 8:16 Isaiah 8:16

Ufunge huo ushuhuda, ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi wangu.

Isaya 8:17 Isaiah 8:17

Nami nitamngojea Bwana, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia.

Isaya 8:18 Isaiah 8:18

Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na Bwana tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa Bwana wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.

Isaya 8:19 Isaiah 8:19

Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?

Isaya 8:20 Isaiah 8:20

Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.

Isaya 8:21 Isaiah 8:21

Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu;

Isaya 8:22 Isaiah 8:22

nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapana changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.