Isaya Mlango 38 Isaiah

Isaya 38:1 Isaiah 38:1

Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

Isaya 38:2 Isaiah 38:2

Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana,

Isaya 38:3 Isaiah 38:3

akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.

Isaya 38:4 Isaiah 38:4

Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema,

Isaya 38:5 Isaiah 38:5

Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.

Isaya 38:6 Isaiah 38:6

Nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu.

Isaya 38:7 Isaiah 38:7

Jambo hili liwe ishara kwako, itokayo kwa Bwana, ya kuwa Bwana atalitimiza jambo hili alilolisema;

Isaya 38:8 Isaiah 38:8

Tazama, nitakirudisha nyuma kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka.

Isaya 38:9 Isaiah 38:9

Haya ndiyo maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda, alipokuwa hawezi, naye akapona ugonjwa wake.

Isaya 38:10 Isaiah 38:10

Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.

Isaya 38:11 Isaiah 38:11

Nalisema, Sitamwona Bwana, yeye Bwana, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.

Isaya 38:12 Isaiah 38:12

Kao langu limeondolewa kabisa, limechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.

Isaya 38:13 Isaiah 38:13

Nalijituliza hata asubuhi; kama simba, aivunja mifupa yangu yote; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.

Isaya 38:14 Isaiah 38:14

Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Naliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee Bwana, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.

Isaya 38:15 Isaiah 38:15

Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.

Isaya 38:16 Isaiah 38:16

Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi; Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote; Kwa hiyo uniponye na kunihuisha.

Isaya 38:17 Isaiah 38:17

Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.

Isaya 38:18 Isaiah 38:18

Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.

Isaya 38:19 Isaiah 38:19

Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto kweli yako.

Isaya 38:20 Isaiah 38:20

Bwana yu tayari kunipa wokovu. Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu, Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa Bwana.

Isaya 38:21 Isaiah 38:21

Maana Isaya amesema, Na watwae mkate wa tini, wakauweke juu ya jipu, naye atapona.

Isaya 38:22 Isaiah 38:22

Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionyesha ya kuwa nitapanda niingie nyumbani mwa Bwana?