Isaya Mlango 21 Isaiah

Isaya 21:1 Isaiah 21:1

Ufunuo juu ya bara ya bahari. Kama tufani za Negebu zikaribiavyo kwa kasi,inakuja kutoka bara,toka nchi itishayo.

Isaya 21:2 Isaiah 21:2

Nimeonyeshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu. Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote.

Isaya 21:3 Isaiah 21:3

Kwa sababu hiyo viuno vyangu vimejaa maumivu, utungu umenishika, kama utungu wa mwanamke azaaye; ninaumwa sana, nisiweze kusikia; nimefadhaishwa wa hofu, nisiweze kuona.

Isaya 21:4 Isaiah 21:4

Moyo wangu unapiga-piga, utisho umenitaabisha, gizagiza la jioni nilipendalo limegeuka likanitetemesha.

Isaya 21:5 Isaiah 21:5

Wanaandika meza, wanaweka ulinzi, wanakula, wanakunywa. Simameni, enyi wakuu, itieni ngao mafuta.

Isaya 21:6 Isaiah 21:6

Maana Bwana ameniambia hivi, Enenda, weka mlinzi; aonayo na ayatangaze.

Isaya 21:7 Isaiah 21:7

Naye akiona kundi la wapanda farasi, wakienda wawili wawili, na kundi la punda, na kundi la ngamia; asikilize sana, akijitahidi kusikiliza.

Isaya 21:8 Isaiah 21:8

Ndipo akalia kama simba, Ee Bwana, mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana, na kila usiku ninakaa katika zamu ya ulinzi wangu.

Isaya 21:9 Isaiah 21:9

Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini.

Isaya 21:10 Isaiah 21:10

Ewe niliyekufikicha, na nafaka ya sakafu yangu; Hayo niliyoyasikia kwa Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, nimewapasha habari zake.

Isaya 21:11 Isaiah 21:11

Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku?

Isaya 21:12 Isaiah 21:12

Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena.

Isaya 21:13 Isaiah 21:13

Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani.

Isaya 21:14 Isaiah 21:14

Waleteeni wenye kiu maji, Enyi wenyeji wa nchi ya Tema; Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao.

Isaya 21:15 Isaiah 21:15

Kwa maana wanakimbia mbele ya panga, Upanga uliofutwa, na upinde uliopindwa, Na mbele ya ukali wa vita.

Isaya 21:16 Isaiah 21:16

Kwa sababu Bwana ameniambia hivi, Katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wote wa Kedari.

Isaya 21:17 Isaiah 21:17

Na mabaki ya hesabu ya wavuta pinde, hao mashujaa wa Kedari watakuwa wachache; maana Bwana, Mungu wa Israeli, amenena neno hili.