Ayabu Mlango 10 Job

Ayabu 10:1 Job 10:1

Nafsi yangu inachoka na maisha yangu; Sitajizuia na kuugua kwangu; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.

Ayabu 10:2 Job 10:2

Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa; Nionyeshe sababu ya wewe kushindana nami.

Ayabu 10:3 Job 10:3

Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuyaangazia mashauri ya waovu?

Ayabu 10:4 Job 10:4

Je! Wewe una macho ya kimwili, Au je! Waona kama aonavyo binadamu?

Ayabu 10:5 Job 10:5

Je! Siku zako ni kama siku za mtu, Au je! Miaka yako ni kama siku za mtu,

Ayabu 10:6 Job 10:6

Hata ukauliza-uliza habari za uovu wangu, Na kuitafuta dhambi yangu,

Ayabu 10:7 Job 10:7

Ujapojua ya kuwa mimi si mwovu; Wala hapana awezaye kuokoa na mkono wako?

Ayabu 10:8 Job 10:8

Mikono yako imeniumba na kunifinyanga; Nawe utageuka na kuniangamiza?

Ayabu 10:9 Job 10:9

Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?

Ayabu 10:10 Job 10:10

Je! Wewe hukunimimina kama maziwa, Na kunigandisha mfano wa jibini?

Ayabu 10:11 Job 10:11

Umenivika ngozi na nyama, Na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa.

Ayabu 10:12 Job 10:12

Umenijazi uhai na upendeleo, Na maangalizi yako yameilinda roho yangu.

Ayabu 10:13 Job 10:13

Lakini mambo haya uliyaficha moyoni mwako; Najua kuwa haya yamo nafsini mwako;

Ayabu 10:14 Job 10:14

Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia, Wala hutaniachilia na uovu wangu.

Ayabu 10:15 Job 10:15

Mimi nikiwa mbaya, ole wangu! Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu; Mimi nimejaa aibu Na kuyaangalia mateso yangu.

Ayabu 10:16 Job 10:16

Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba; Tena wajionyesha kwangu kuwa wa ajabu.

Ayabu 10:17 Job 10:17

Wewe warejeza upya hao mashahidi yako juu yangu, Na kasirani yako waiongeza juu yangu; Jeshi kwa jeshi juu yangu.

Ayabu 10:18 Job 10:18

Kwa nini basi kunitoa tumboni? Ningekata roho, lisinione jicho lo lote.

Ayabu 10:19 Job 10:19

Ningalikuwa kama mtu asiyekuwapo; Ningalichukuliwa kaburini kutoka tumboni.

Ayabu 10:20 Job 10:20

Je! Siku zangu si chache? Acha basi, Usinisumbue, nipate ngaa kutuzwa moyo kidogo.

Ayabu 10:21 Job 10:21

Kabla sijaenda huko ambako sitarudi kutoka huko tena, Ni hiyo nchi ya giza, giza tupu;

Ayabu 10:22 Job 10:22

Ni nchi ya giza kuu, kama giza lenyewe lilivyo; Ni nchi ya giza tupu, isiyo na matengezo ya mambo yo yote, Nchi ambayo nuru yake ni kama giza.