Ayabu Mlango 37 Job

Ayabu 37:1 Job 37:1

Moyo wangu hunitetema kwayo pia, Nao hutoka mahali pake.

Ayabu 37:2 Job 37:2

Zisikizeni hizo kelele za sauti yake, Na uvumi utokao kinywani mwake.

Ayabu 37:3 Job 37:3

Yeye huituma iende chini ya mbingu zote, Na radi yake hata miisho ya nchi.

Ayabu 37:4 Job 37:4

Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.

Ayabu 37:5 Job 37:5

Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuelewa nayo.

Ayabu 37:6 Job 37:6

Kwani huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na vivyo manyonyota ya mvua, Na hayo maji ya mvua yake kubwa.

Ayabu 37:7 Job 37:7

Huufunga mkono wa kila binadamu; Ili watu wote aliowaumba wajue.

Ayabu 37:8 Job 37:8

Hapo wanyama huingia mafichoni, Na kukaa katika mapango yao.

Ayabu 37:9 Job 37:9

Dhoruba hutoka katika vyumba vyake; Na baridi ghalani mwake.

Ayabu 37:10 Job 37:10

Barafu huletwa kwa pumzi za Mungu; Na upana wa maji huganda.

Ayabu 37:11 Job 37:11

Naam, huyatweka mawingu mazito mzigo wa maji; Hulitandika wingu la umeme wake;

Ayabu 37:12 Job 37:12

Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake, Ili yafanye yote atakayoyaagiza Juu ya uso wa dunia hii ikaayo watu;

Ayabu 37:13 Job 37:13

Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake, Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye.

Ayabu 37:14 Job 37:14

Sikiliza neno hili, Ee Ayubu; Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu.

Ayabu 37:15 Job 37:15

Je! Wajua wewe jinsi Mungu anavyoziagiza, Na kuumulikisha umeme wa wingu lake?

Ayabu 37:16 Job 37:16

Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?

Ayabu 37:17 Job 37:17

Jinsi nguo zako zilivyo na moto, Hapo nchi ituliapo kwa sababu ya upepo wa kusini?

Ayabu 37:18 Job 37:18

Je! Waweza kuzitandaza mbingu pamoja naye, Ambazo zina nguvu kama kioo cha kuyeyushwa?

Ayabu 37:19 Job 37:19

Utufundishe ni maneno gani tutakayomwambia; Kwa maana hamwezi kuyatengeza kwa sababu ya giza.

Ayabu 37:20 Job 37:20

Je! Aambiwe kwamba nataka kunena? Au mtu angetamani kumezwa?

Ayabu 37:21 Job 37:21

Na sasa watu hawawezi kuutazama mwanga ung'aao mbinguni; Lakini upepo ukipita huzitakasa.

Ayabu 37:22 Job 37:22

Kaskazini hutokea umemetufu wa dhahabu; Mungu huvikwa ukuu utishao.

Ayabu 37:23 Job 37:23

yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.

Ayabu 37:24 Job 37:24

Kwa hiyo watu humwogopa; Yeye hawaangalii walio na hekima mioyoni.