Ayabu Mlango 7 Job

Ayabu 7:1 Job 7:1

Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa?

Ayabu 7:2 Job 7:2

Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake;

Ayabu 7:3 Job 7:3

Ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha.

Ayabu 7:4 Job 7:4

Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke.

Ayabu 7:5 Job 7:5

Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena.

Ayabu 7:6 Job 7:6

Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.

Ayabu 7:7 Job 7:7

Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena.

Ayabu 7:8 Job 7:8

Jicho lake huyo anionaye halitaniangalia tena; Macho yako yatanielekea, lakini sitakuwapo.

Ayabu 7:9 Job 7:9

Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.

Ayabu 7:10 Job 7:10

Hatarudi tena nyumbani kwake, Wala mahali pake hapatamjua tena.

Ayabu 7:11 Job 7:11

Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitanena kwa mateso ya roho yangu; Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu.

Ayabu 7:12 Job 7:12

Je! Mimi ni bahari, au je! Ni nyangumi? Hata ukawaweka walinzi juu yangu?

Ayabu 7:13 Job 7:13

Hapo nisemapo, kitanda changu kitanituza moyo, Malazi yangu yatanipunguzia kuugua kwangu;

Ayabu 7:14 Job 7:14

Ndipo unitishapo kwa ndoto, Na kunitia hofu kwa maono;

Ayabu 7:15 Job 7:15

Hata nafsi yangu huchagua kunyongwa, Na kuchagua kifo kuliko maumivu yangu haya.

Ayabu 7:16 Job 7:16

Ninadhoofika; sitaishi sikuzote; Usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio.

Ayabu 7:17 Job 7:17

Je! Mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza, Na kumtia moyoni mwako,

Ayabu 7:18 Job 7:18

Na kumwangalia kila asubuhi, Na kumjaribu kila dakika?

Ayabu 7:19 Job 7:19

Je! Hata lini hukomi kuniangalia; Wala kunisumbua hata nimeze mate?

Ayabu 7:20 Job 7:20

Kwamba nimefanya dhambi, nikufanyieje Ee mlinda wanadamu? Mbona umeniweka niwe shabaha yako, Hata nimekuwa mzigo kwa nafsi yangu?

Ayabu 7:21 Job 7:21

Nawe, je! Mbona hunisamehe makosa yangu, Na kuniondolea maovu yangu? Kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; Nawe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwapo.