Ayabu Mlango 21 Job

Ayabu 21:1 Job 21:1

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

Ayabu 21:2 Job 21:2

Yasikizeni sana maneno yangu; Jambo hili na liwe faraja yenu.

Ayabu 21:3 Job 21:3

Niacheni, nami pia nitanena; Tena nikiisha nena, zidini kudhihaki.

Ayabu 21:4 Job 21:4

Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu? Nami kwa nini nisikose kusubiri?

Ayabu 21:5 Job 21:5

Niangalieni, mkastaajabu, Mkaweke mkono kinywani.

Ayabu 21:6 Job 21:6

Hata nikumbukapo nahuzunika, Na utisho wanishika mwilini mwangu.

Ayabu 21:7 Job 21:7

Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?

Ayabu 21:8 Job 21:8

Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao.

Ayabu 21:9 Job 21:9

Nyumba zao zi salama pasina hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi.

Ayabu 21:10 Job 21:10

Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng'ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba.

Ayabu 21:11 Job 21:11

Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza.

Ayabu 21:12 Job 21:12

Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi.

Ayabu 21:13 Job 21:13

Siku zao hutumia katika kufanikiwa, Kisha hushuka kuzimuni ghafula.

Ayabu 21:14 Job 21:14

Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako.

Ayabu 21:15 Job 21:15

Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?

Ayabu 21:16 Job 21:16

Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao; Mashauri ya waovu na yawe mbali nami.

Ayabu 21:17 Job 21:17

Je! Ni mara ngapi taa yao waovu huzimishwa? Na msiba wao kuwajilia? Na Mungu kuwagawanyia uchungu kwa hasira yake?

Ayabu 21:18 Job 21:18

Ili wawe kama mabua makavu mbele ya upepo, Kama makapi yaliyochukuliwa na dhoruba?

Ayabu 21:19 Job 21:19

Mwasema, Mungu huwawekea watoto wa mtu huo uovu wake. Na amlipe mwenyewe, ili apate kuujua.

Ayabu 21:20 Job 21:20

Macho yake mwenyewe na yaone uharibifu wake, Akanywe ghadhabu zake Mwenyezi.

Ayabu 21:21 Job 21:21

Kwani ana furaha gani katika mbari yake baada yake, Hesabu ya miezi yake itakapokwisha katwa katikati?

Ayabu 21:22 Job 21:22

Je! Mtu awaye yote atamfundisha Mungu maarifa? Naye ndiye awahukumuye walioko juu.

Ayabu 21:23 Job 21:23

Mmoja hufa katika nguvu zake kamili, Mwenye kukaa salama na kustarehe;

Ayabu 21:24 Job 21:24

Vyombo vyake vimejaa maziwa, Na mafuta ya mifupani mwake ni laini.

Ayabu 21:25 Job 21:25

Mwingine hufa katika uchungu wa roho, Asionje mema kamwe.

Ayabu 21:26 Job 21:26

Wao hulala mavumbini sawasawa, Mabuu huwafunika.

Ayabu 21:27 Job 21:27

Tazama, nayajua mawazo yenu, Na mashauri mnayoazimia kwa uovu juu yangu.

Ayabu 21:28 Job 21:28

Kwa kuwa mwasema, Nyumba ya huyo mkuu i wapi? Na hema waliyoikaa hao waovu i wapi?

Ayabu 21:29 Job 21:29

Je! Hamkuwauliza wapitao njiani? Na maonyo yao hamyajui?

Ayabu 21:30 Job 21:30

Kwamba mwovu huachiliwa katika siku ya msiba? Na kuongozwa nje katika siku ya ghadhabu?

Ayabu 21:31 Job 21:31

Ni nani atakayetangaza njia yake usoni pake? Tena ni nani atakayemlipa kwa hayo aliyofanya?

Ayabu 21:32 Job 21:32

Pamoja na hayo atachukuliwa kaburini, Nao watalinda zamu juu ya ziara lake.

Ayabu 21:33 Job 21:33

Udongo wa bondeni utakuwa tamu kwake, Na watu wote watafuata nyuma yake, Kama vile walivyomtangulia watu wasiohesabika.

Ayabu 21:34 Job 21:34

Basi imekuwaje ninyi kunituza moyo bure, Kwa kuwa katika jawabu zenu unasalia uongo tu.