Ayabu Mlango 31 Job

Ayabu 31:1 Job 31:1

Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?

Ayabu 31:2 Job 31:2

Kwani sehemu ya Mungu itokayo juu ingekuwa nini, Na urithi wa Mwenyezi utokao juu?

Ayabu 31:3 Job 31:3

Je! Siyo msiba kwa wasio haki, Na hasara kwao watendao uovu?

Ayabu 31:4 Job 31:4

Je! Yeye hazioni njia zangu, Na kuzihesabu hatua zangu zote?

Ayabu 31:5 Job 31:5

Kwamba nimetembea katika ubatili, Na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu;

Ayabu 31:6 Job 31:6

(Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu wangu);

Ayabu 31:7 Job 31:7

Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, Na moyo wangu kuyaandama macho yangu, Tena kwamba kipaku cho chote kimeshikamana na mikono yangu;

Ayabu 31:8 Job 31:8

Basi na nipande, mwingine ale; Naam, mazao ya shamba langu na yang'olewe.

Ayabu 31:9 Job 31:9

Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke, Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;

Ayabu 31:10 Job 31:10

Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine, Na wengine na wainame juu yake.

Ayabu 31:11 Job 31:11

Kwani hilo lingekuwa kosa kuu; Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;

Ayabu 31:12 Job 31:12

Kwa kuwa ni moto uteketezao hata Uharibifu, Nao ungeyang'oa maongeo yangu yote.

Ayabu 31:13 Job 31:13

Kama nimeidharau daawa ya mtumishi wangu, au ya kijakazi changu, Waliposhindana nami;

Ayabu 31:14 Job 31:14

Basi Mungu atakapoinuka nitafanya nini? Naye atakapozuru, nitamjibuje?

Ayabu 31:15 Job 31:15

Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?

Ayabu 31:16 Job 31:16

Ikiwa nimewanyima maskini haja zao, Au kama nimeyatia kiwi macho ya mwanamke mjane;

Ayabu 31:17 Job 31:17

Au kama nimekula tonge langu peke yangu, Mayatima wasipate kulila;

Ayabu 31:18 Job 31:18

(La, tangu ujana wangu alikua pamoja nami kama kwa baba; Nami nimekuwa ni kiongozi cha mjane tangu tumbo la mamangu);

Ayabu 31:19 Job 31:19

Ikiwa nimemwona mtu kuangamia kwa kukosa nguo, Au wahitaji kukosa mavazi;

Ayabu 31:20 Job 31:20

Ikiwa viuno vyake havikunibarikia, Au kama hakupata moto kwa manyoya ya kondoo zangu;

Ayabu 31:21 Job 31:21

Ikiwa nimewainulia mayatima mkono, Nilipoona msaada wangu langoni;

Ayabu 31:22 Job 31:22

Basi bega langu na lianguke kutoka mahali pake, Na mkono wangu uvunjike mfupani mwake.

Ayabu 31:23 Job 31:23

Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu, Na kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.

Ayabu 31:24 Job 31:24

Ikiwa nimeifanya dhahabu kuwa tumaini langu, Na kuiambia dhahabu safi, Wewe u tegemeo langu;

Ayabu 31:25 Job 31:25

Kama nilifurahi kwa kuwa mali yangu yalikuwa mengi, Na kwa sababu mkono wangu umepata vitu vingi;

Ayabu 31:26 Job 31:26

Kama nililitazama jua lilipoangaza, Au mwezi ukiendelea katika kung'aa;

Ayabu 31:27 Job 31:27

Na moyo wangu umeshawishwa kwa siri, Na midomo yangu imeubusu mkono wangu;

Ayabu 31:28 Job 31:28

Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi; Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu.

Ayabu 31:29 Job 31:29

Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia, Au kujitukuza alipopatikana na maovu;

Ayabu 31:30 Job 31:30

(Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza);

Ayabu 31:31 Job 31:31

Kama watu wa hemani mwangu hawakunena, Ni nani awezaye kumpata mtu asiyeshibishwa na yeye kwa nyama?

Ayabu 31:32 Job 31:32

Mgeni hakulala njiani; Lakini nilimfungulia msafiri milango yangu;

Ayabu 31:33 Job 31:33

Ikiwa kama mwanadamu nimeyafunika makosa yangu, Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu;

Ayabu 31:34 Job 31:34

Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa, Na dharau la jamaa lilinitia hofu, Hata nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni-

Ayabu 31:35 Job 31:35

Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu); Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu!

Ayabu 31:36 Job 31:36

Hakika ningeyachukua mabegani; Ningejifungia mfano wa kilemba.

Ayabu 31:37 Job 31:37

Ningemwambia hesabu ya hatua zangu Ningemkaribia kama vile mkuu.

Ayabu 31:38 Job 31:38

Kama nchi yangu yalia juu yangu, Na matuta yake hulia pamoja;

Ayabu 31:39 Job 31:39

Kama nimeyala matunda yake pasipo kulipa, Au kama nimewafanya wenyewe kupotewa na uhai;

Ayabu 31:40 Job 31:40

Miiba na imee badala ya ngano, Na magugu badala ya shayiri. Maneno ya Ayubu yamekoma hapa.