Ayabu Mlango 6 Job

Ayabu 6:1 Job 6:1

Ndipo Ayubu akajibu na kusema,

Ayabu 6:2 Job 6:2

Laiti uchungu wangu ungepimwa, Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja!

Ayabu 6:3 Job 6:3

Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari; Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.

Ayabu 6:4 Job 6:4

Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi i ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.

Ayabu 6:5 Job 6:5

Je! Huyo punda-mwitu hulia akiwa na majani? Au, ng'ombe hulia malishoni?

Ayabu 6:6 Job 6:6

Je! Kitu kisicho na ladha yumkini kulika pasipo chumvi? Au je, uto wa yai una tamu iwayo yote?

Ayabu 6:7 Job 6:7

Roho yangu inakataa hata kuvigusa; Kwangu mimi ni kama chakula kichukizacho.

Ayabu 6:8 Job 6:8

Laiti ningepewa haja yangu, Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana!

Ayabu 6:9 Job 6:9

Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniseta; Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!

Ayabu 6:10 Job 6:10

Hapo ndipo ningefarijika hata sasa; Naam, ningejikuza katika maumivu yasiyoniacha; Kwa kuwa sikuyakana maneno yake Mtakatifu.

Ayabu 6:11 Job 6:11

Nguvu zangu ni zipi, hata ningoje? Na mwisho wangu ni nini, hata nisubiri?

Ayabu 6:12 Job 6:12

Je! Nguvu zangu ni nguvu za mawe? Au mwili wangu, je! Ni shaba?

Ayabu 6:13 Job 6:13

Je! Si kwamba sina msaada ndani yangu. Tena kwamba kufanikiwa kumeondolewa mbali nami?

Ayabu 6:14 Job 6:14

Kwake huyo atakaye kuzima roho inapasa atendewe mema na rafiki; Hata kwake huyo aachaye kumcha Mwenyezi.

Ayabu 6:15 Job 6:15

Ndugu zangu wametenda udanganyifu kama kijito cha maji. Mfano wa fumbi la vijito vipitavyo.

Ayabu 6:16 Job 6:16

Vilivyokuwa vyeusi kwa sababu ya barafu, Ambamo theluji hujificha.

Ayabu 6:17 Job 6:17

Wakati vipatapo moto hutoweka; Kukiwako hari, hukoma mahali pao.

Ayabu 6:18 Job 6:18

Misafara isafiriyo kwa njia yao hugeuka; Hukwea kwenda barani, na kupotea.

Ayabu 6:19 Job 6:19

Misafara ya Tema huvitazama, Majeshi ya Sheba huvingojea.

Ayabu 6:20 Job 6:20

Wametahayari kwa sababu walitumaini; Wakaja huku, nao walifadhaika.

Ayabu 6:21 Job 6:21

Kwani sasa ninyi mmekuwa vivyo; Mwaona jambo la kutisha, mkaogopa.

Ayabu 6:22 Job 6:22

Je! Nilisema, Nipeni? Au, Nitoleeni toleo katika mali yenu?

Ayabu 6:23 Job 6:23

Au, Niokoeni na mkono wa adui? Au, Nikomboeni na mikono ya hao waoneao?

Ayabu 6:24 Job 6:24

Nifunzeni, nami nitanyamaa kimya; Mkanijulishe ni jambo gani nililokosa.

Ayabu 6:25 Job 6:25

Jinsi yafaavyo maneno ya uelekevu! Lakini kuhoji kwenu, je! Kumeonya nini?

Ayabu 6:26 Job 6:26

Je! Mwafikiri kuyakemea maneno? Maana maneno ya huyo aliyekata tamaa ni kama upepo.

Ayabu 6:27 Job 6:27

Naam, mwapenda kuwapigia kura hao mayatima, Na kufanya biashara ya rafiki yenu.

Ayabu 6:28 Job 6:28

Sasa basi iweni radhi kuniangalia; Kwani hakika sitanena uongo usoni penu.

Ayabu 6:29 Job 6:29

Rudini, nawasihi, lisiwe neno la udhalimu; Naam, rudini tena, neno langu ni la haki.

Ayabu 6:30 Job 6:30

Je! Mna udhalimu ulimini mwangu? Je! Makaakaa yangu hayatambui mambo ya madhara?