Ayabu Mlango 14 Job

Ayabu 14:1 Job 14:1

Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.

Ayabu 14:2 Job 14:2

Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.

Ayabu 14:3 Job 14:3

Nawe, je! Wafumbua macho yako kumwangalia mtu kama yeye, Na kunitia katika hukumu pamoja nawe?

Ayabu 14:4 Job 14:4

Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye.

Ayabu 14:5 Job 14:5

Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;

Ayabu 14:6 Job 14:6

Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika, Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa.

Ayabu 14:7 Job 14:7

Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma.

Ayabu 14:8 Job 14:8

Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo;

Ayabu 14:9 Job 14:9

Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche.

Ayabu 14:10 Job 14:10

Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?

Ayabu 14:11 Job 14:11

Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika;

Ayabu 14:12 Job 14:12

Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.

Ayabu 14:13 Job 14:13

Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka!

Ayabu 14:14 Job 14:14

Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za vita vyangu, Hata kufunguliwa kwangu kunifikilie.

Ayabu 14:15 Job 14:15

Wewe ungeita, nami ningekujibu; Ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako.

Ayabu 14:16 Job 14:16

Lakini sasa wazihesabu hatua zangu; Je! Huchungulii dhambi yangu?

Ayabu 14:17 Job 14:17

Kosa langu limetiwa muhuri mfukoni, Nawe waufunga uovu wangu.

Ayabu 14:18 Job 14:18

Lakini, tazama, mlima ukianguka hutoweka, Nalo jabali huondolewa mahali pake;

Ayabu 14:19 Job 14:19

Maji mengi huyapunguza mawe; Mafuriko yake huuchukua mchanga wa nchi; Nawe matumaini ya wanadamu wayaangamiza.

Ayabu 14:20 Job 14:20

Wewe wamshinda nguvu sikuzote, naye hupita aende zake Wabadili sura zake, na kumpeleka aondoke.

Ayabu 14:21 Job 14:21

Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.

Ayabu 14:22 Job 14:22

Lakini mwili ulio juu yake una maumivu, Na nafsi yake ndani huomboleza.