Ayabu Mlango 4 Job

Ayabu 4:1 Job 4:1

Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema,

Ayabu 4:2 Job 4:2

Mtu akijaribu kuzungumza nawe, je! Utaona ni vibaya? Lakini ni nani awezaye kujizuia asinene?

Ayabu 4:3 Job 4:3

Tazama, wewe umewafunza watu wengi, Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge.

Ayabu 4:4 Job 4:4

Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge.

Ayabu 4:5 Job 4:5

Lakini sasa haya yamekufikilia wewe, nawe wafa moyo; Yamekugusa, nawe wafadhaika.

Ayabu 4:6 Job 4:6

Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?

Ayabu 4:7 Job 4:7

Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi?

Ayabu 4:8 Job 4:8

Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.

Ayabu 4:9 Job 4:9

Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika.

Ayabu 4:10 Job 4:10

Kunguruma kwake simba, na sauti ya simba mkali, Na meno ya simba wachanga, yamevunjika.

Ayabu 4:11 Job 4:11

Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo, Nao watoto wa simba mke wametawanyika mbalimbali.

Ayabu 4:12 Job 4:12

Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake.

Ayabu 4:13 Job 4:13

Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.

Ayabu 4:14 Job 4:14

Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote.

Ayabu 4:15 Job 4:15

Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama.

Ayabu 4:16 Job 4:16

Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,

Ayabu 4:17 Job 4:17

Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu? Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?

Ayabu 4:18 Job 4:18

Tazama, yeye hawategemei watumishi wake; Na malaika zake huwahesabia upuzi;

Ayabu 4:19 Job 4:19

Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo, Ambazo misingi yao i katika mchanga, Hao waliosetwa mbele ya nondo!

Ayabu 4:20 Job 4:20

Kati ya asubuhi na jioni huvunjwa-vunjwa; Waangamia milele wala hapana atiaye moyoni.

Ayabu 4:21 Job 4:21

Je! Kamba ya hema yao haikung'olewa ndani yao? Wafa, kisha hali hawana akili.