Ayabu Mlango 33 Job

Ayabu 33:1 Job 33:1

Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu, Ukayasikilize maneno yangu yote.

Ayabu 33:2 Job 33:2

Tazama basi, nimefunua kinywa changu, Ulimi wangu umenena kinywani mwangu.

Ayabu 33:3 Job 33:3

Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu; Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.

Ayabu 33:4 Job 33:4

Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.

Ayabu 33:5 Job 33:5

Kwamba waweza, nijibu; Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.

Ayabu 33:6 Job 33:6

Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe; Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.

Ayabu 33:7 Job 33:7

Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe, Wala sitakulemea kwa uzito.

Ayabu 33:8 Job 33:8

Hakika umenena masikioni mwangu, Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema,

Ayabu 33:9 Job 33:9

Mimi ni safi, sina makosa; Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu;

Ayabu 33:10 Job 33:10

Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami, Hunihesabu kuwa ni adui yake;

Ayabu 33:11 Job 33:11

Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza.

Ayabu 33:12 Job 33:12

Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki; Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.

Ayabu 33:13 Job 33:13

Nawe kwani kumnung'unikia, Kwa vile asivyotoa hesabu ya mambo yake yote?

Ayabu 33:14 Job 33:14

Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.

Ayabu 33:15 Job 33:15

Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;

Ayabu 33:16 Job 33:16

Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,

Ayabu 33:17 Job 33:17

Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;

Ayabu 33:18 Job 33:18

Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.

Ayabu 33:19 Job 33:19

Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;

Ayabu 33:20 Job 33:20

Hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri.

Ayabu 33:21 Job 33:21

Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane; Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje.

Ayabu 33:22 Job 33:22

Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi.

Ayabu 33:23 Job 33:23

Kwamba akiwapo malaika pamoja naye, Mkalimani, mmoja katika elfu, Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo;

Ayabu 33:24 Job 33:24

Ndipo amwoneapo rehema, na kusema, Mwokoe asishuke shimoni; Mimi nimeuona ukombozi.

Ayabu 33:25 Job 33:25

Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto; Huzirudia siku za ujana wake;

Ayabu 33:26 Job 33:26

Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia; Hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejezea mtu haki yake.

Ayabu 33:27 Job 33:27

Yeye huimba mbele ya watu, na kusema, Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea, Wala sikulipizwa jambo hilo;

Ayabu 33:28 Job 33:28

Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga.

Ayabu 33:29 Job 33:29

Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya, Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu,

Ayabu 33:30 Job 33:30

Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.

Ayabu 33:31 Job 33:31

Angalia sana, Ee Ayubu, unisikilize; Nyamaza, mimi nitasema.

Ayabu 33:32 Job 33:32

Kama una neno la kusema, nijibu; Nena, kwani nataka kukuhesabia kuwa na haki.

Ayabu 33:33 Job 33:33

Kama sivyo, unisikilize mimi; Nyamaza, nami nitakufunza hekima.