Ayabu Mlango 17 Job

Ayabu 17:1 Job 17:1

Roho yangu imezimika, siku zangu zimekoma, Kaburi i tayari kunipokea.

Ayabu 17:2 Job 17:2

Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka, Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao.

Ayabu 17:3 Job 17:3

Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe; Kuna nani atakayeniwekea dhamana?

Ayabu 17:4 Job 17:4

Kwani mioyo yao imeificha ufahamu; Kwa hiyo hutawakuza.

Ayabu 17:5 Job 17:5

Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo, Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi.

Ayabu 17:6 Job 17:6

Amenifanya niwe simo kwa watu; Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.

Ayabu 17:7 Job 17:7

Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.

Ayabu 17:8 Job 17:8

Walekevu watayastaajabia hayo, Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu.

Ayabu 17:9 Job 17:9

Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.

Ayabu 17:10 Job 17:10

Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa; Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu.

Ayabu 17:11 Job 17:11

Siku zangu zimepita, makusudi yangu yamevunjika, Hata hayo niliyo nayo moyoni mwangu.

Ayabu 17:12 Job 17:12

Wabadili usiku kuwa mchana; Wasema, Mwanga u karibu kwa sababu ya giza.

Ayabu 17:13 Job 17:13

Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu; Nikitandika malazi yangu gizani;

Ayabu 17:14 Job 17:14

Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu; Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na umbu langu;

Ayabu 17:15 Job 17:15

Basi, tumaini langu li wapi? Na tumaini langu, ni nani atakayeliona?

Ayabu 17:16 Job 17:16

Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu, Itakapokuwapo raha mavumbini.