Ayabu Mlango 22 Job

Ayabu 22:1 Job 22:1

Ndipo huyo Elifazi Mtemani akajibu, na kusema,

Ayabu 22:2 Job 22:2

Je! Yumkini mtu awaye yote kumfaa Mungu? Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe.

Ayabu 22:3 Job 22:3

Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu?

Ayabu 22:4 Job 22:4

Je! Ni kwa wewe kumcha yeye anakukemea? Na kuingia hukumuni nawe?

Ayabu 22:5 Job 22:5

Je! Uovu wako si mkuu? Wala maovu yako hayana mwisho.

Ayabu 22:6 Job 22:6

Kwa kuwa umetwaa dhamana kwa nduguyo bure, Na kuwavua nguo zao walio uchi.

Ayabu 22:7 Job 22:7

Hukumpa maji ya kunywa huyo aliyechoka, Nawe umemnyima chakula huyo mwenye njaa.

Ayabu 22:8 Job 22:8

Lakini huyo shujaa, nchi ilikuwa yake; Na huyo mwenye kusifiwa, yeye aliikaa.

Ayabu 22:9 Job 22:9

Umewafukuza wanawake wajane hali ya utupu, Na mikono ya mayatima imevunjwa.

Ayabu 22:10 Job 22:10

Kwa hiyo umezungukwa na mitego, Na hofu ya ghafula yakutaabisha,

Ayabu 22:11 Job 22:11

Au je! Huoni giza, Na maji mengi yanayokufunika?

Ayabu 22:12 Job 22:12

Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu!

Ayabu 22:13 Job 22:13

Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu?

Ayabu 22:14 Job 22:14

Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu.

Ayabu 22:15 Job 22:15

Je! Utaiandama njia ya zamani Waliyoikanyaga watu waovu?

Ayabu 22:16 Job 22:16

Ambao walinyakuliwa kabla ya wakati wao, Msingi wao ulimwagika kama kijito cha maji;

Ayabu 22:17 Job 22:17

Waliomwambia Mungu, Tuondokee; Tena, Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?

Ayabu 22:18 Job 22:18

Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema; Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.

Ayabu 22:19 Job 22:19

Wenye haki huyaona hayo wakafurahi; Nao wasio na hatia huwacheka;

Ayabu 22:20 Job 22:20

Wasema, Hakika hao waliotuinukia wamekatiliwa mbali, Na mabaki yao moto umeyateketeza.

Ayabu 22:21 Job 22:21

Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.

Ayabu 22:22 Job 22:22

Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako.

Ayabu 22:23 Job 22:23

Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa; Ukiuondoa udhalimu mbali na hema yako.

Ayabu 22:24 Job 22:24

Nawe hazina zako ziweke mchangani, Na dhahabu ya Ofiri iweke kati ya mawe ya vijito;

Ayabu 22:25 Job 22:25

Naye Mwenyezi atakuwa hazina yako, Atakuwa ni fedha ya thamani kwako.

Ayabu 22:26 Job 22:26

Kwani ndipo utakapojifurahisha katika Mwenyezi, Na kuinua uso wako kumwelekea Mungu.

Ayabu 22:27 Job 22:27

Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako.

Ayabu 22:28 Job 22:28

Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako.

Ayabu 22:29 Job 22:29

Hapo watakapokuangusha, utasema, Kuna kuinuka tena; Naye mnyenyekevu Mungu atamwokoa.

Ayabu 22:30 Job 22:30

Atamwokoa na huyo asiye na hatia; Naam, utaokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.