Ayabu Mlango 29 Job

Ayabu 29:1 Job 29:1

Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema,

Ayabu 29:2 Job 29:2

Laiti ningekuwa kama nilivyokuwa katika miezi ya kale, Kama katika siku hizo Mungu aliponilinda;

Ayabu 29:3 Job 29:3

Hapo taa yake ilipomulika juu yangu kichwani, Nami nilitembea gizani kwa njia ya mwanga wake;

Ayabu 29:4 Job 29:4

Kama nilivyokuwa katika siku zangu za kukomaa, Hapo siri ya Mungu ilipokuwa hemani mwangu;

Ayabu 29:5 Job 29:5

Wakati Mwenyezi alipokuwa akali pamoja nami, Nao watoto wangu walipokuwa wakinizunguka;

Ayabu 29:6 Job 29:6

Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi, Nalo jabali liliponimiminia mito ya mafuta!

Ayabu 29:7 Job 29:7

Wakati nilipotoka kwenda mjini, hata langoni, Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,

Ayabu 29:8 Job 29:8

Hao vijana waliniona wakajificha, Nao wazee wakaniondokea na kusimama;

Ayabu 29:9 Job 29:9

Wakuu wakanyamaa wasinene, Na kuweka mikono yao vinywani mwao;

Ayabu 29:10 Job 29:10

Sauti yao masheki ilinyamaa, Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao.

Ayabu 29:11 Job 29:11

Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia.

Ayabu 29:12 Job 29:12

Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.

Ayabu 29:13 Job 29:13

Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.

Ayabu 29:14 Job 29:14

Nalijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.

Ayabu 29:15 Job 29:15

Nalikuwa macho kwa kipofu, Nalikuwa miguu kwa aliyechechemea.

Ayabu 29:16 Job 29:16

Nalikuwa baba kwa mhitaji, Na daawa ya mtu nisiyemjua naliichunguza.

Ayabu 29:17 Job 29:17

Nami nilizivunja taya za wasio haki, Na kumpokonya mawindo katika meno yake.

Ayabu 29:18 Job 29:18

Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kioto changu, Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga;

Ayabu 29:19 Job 29:19

Shina langu limeenea hata kufika majini, Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu;

Ayabu 29:20 Job 29:20

Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu.

Ayabu 29:21 Job 29:21

Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja, Wakanyamaa kimya wapate sikia mashauri yangu.

Ayabu 29:22 Job 29:22

Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu; Matamko yangu yakadondoka juu yao.

Ayabu 29:23 Job 29:23

Walikuwa wakiningojea kama kungojea mvua; Wakafunua vinywa vyao sana kama mvua ya masika.

Ayabu 29:24 Job 29:24

Walipokata tamaa nikacheka nao; Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha.

Ayabu 29:25 Job 29:25

Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao. Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari, Mfano wa awafarijiye hao waombolezao.