Ayabu Mlango 40 Job

Ayabu 40:1 Job 40:1

Bwana akafuliza kumjibu Ayubu, na kusema,

Ayabu 40:2 Job 40:2

Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.

Ayabu 40:3 Job 40:3

Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema,

Ayabu 40:4 Job 40:4

Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini? Naweka mkono wangu kinywani pangu.

Ayabu 40:5 Job 40:5

Nimenena mara moja, nami sitajibu; Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.

Ayabu 40:6 Job 40:6

Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,

Ayabu 40:7 Job 40:7

Jifunge viuno kama mwanamume, Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie.

Ayabu 40:8 Job 40:8

Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?

Ayabu 40:9 Job 40:9

Au je! Wewe una mkono kama Mungu? Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye?

Ayabu 40:10 Job 40:10

Haya! Jivike sasa fahari na ukuu; Jipambe heshima na enzi.

Ayabu 40:11 Job 40:11

Mwaga mafuriko ya hasira zako, Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili.

Ayabu 40:12 Job 40:12

Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe, Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo.

Ayabu 40:13 Job 40:13

Wafiche mavumbini pamoja, Wafunge nyuso zao mahali palipositirika.

Ayabu 40:14 Job 40:14

Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako, Ya kuwa mkono wako wa kuume waweza kukuokoa.

Ayabu 40:15 Job 40:15

Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe; Yeye hula nyasi kama vile ng'ombe,

Ayabu 40:16 Job 40:16

Tazama basi, nguvu zake ni katika viuno vyake, Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake.

Ayabu 40:17 Job 40:17

Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi; Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.

Ayabu 40:18 Job 40:18

Mifupa yake ni kama mirija ya shaba; Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.

Ayabu 40:19 Job 40:19

Yeye ni mkuu wa njia za Mungu; Yeye aliyemfanya alimpa upanga wake.

Ayabu 40:20 Job 40:20

Hakika milima humtolea chakula; Hapo wachezapo wanyama wote wa barani.

Ayabu 40:21 Job 40:21

Hulala chini ya miti yenye vivuli, Mafichoni penye mianzi, na matopeni.

Ayabu 40:22 Job 40:22

Hiyo miti yenye vivuli humfunika kwa vivuli vyao; Mierebi ya vijito humzunguka.

Ayabu 40:23 Job 40:23

Tazama, mto ukifurika, yeye hatetemeki; Hujiona yu salama, ijapokuwa Yordani hufurika hata kinywani pake.

Ayabu 40:24 Job 40:24

Je! Mtu ye yote atamnasa akiwa yu macho, Au, kumtoboa pua yake kwa mtego?