Ayabu Mlango 32 Job

Ayabu 32:1 Job 32:1

Basi hao watu watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa sababu alikuwa mwenye haki machoni pake mwenyewe.

Ayabu 32:2 Job 32:2

Ndipo zikawaka hasira za huyo Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, katika jamaa ya Ramu, juu ya Ayubu, kwa sababu alikuwa amejipa haki mwenyewe zaidi ya Mungu.

Ayabu 32:3 Job 32:3

Tena hasira zake ziliwaka juu ya hao rafiki zake watatu kwa sababu hawakupata jawabu, lakini wamemhukumia Ayubu makosa.

Ayabu 32:4 Job 32:4

Basi huyo Elihu alikuwa anangoja ili anene na Ayubu, kwa sababu hao wengine walikuwa wazee kuliko yeye.

Ayabu 32:5 Job 32:5

Hata Elihu alipoona kuwa hapana jawabu katika vinywa vya watu hao watatu, hasira zake ziliwaka.

Ayabu 32:6 Job 32:6

Basi Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, akajibu, na kusema, Mimi ni kijana, na ninyi ni wazee sana; Kwa hiyo nilijizuia, nisithubutu kuwaonyesha nionavyo.

Ayabu 32:7 Job 32:7

Nilisema, Yafaa siku ziseme, Na wingi wa miaka ufundishe hekima.

Ayabu 32:8 Job 32:8

Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.

Ayabu 32:9 Job 32:9

Sio wakuu walio wenye akili, Wala sio wazee watambuao hukumu.

Ayabu 32:10 Job 32:10

Basi nilisema, Nisikilizeni mimi; Mimi nami nitawaonyesha nionavyo.

Ayabu 32:11 Job 32:11

Tazama, niliyangojea maneno yenu, Nilizisikiliza nisikie hoja zenu, Hapo mlipokitafuta mtakalonena.

Ayabu 32:12 Job 32:12

Naam, niliwasikiza ninyi, Na tazama, hapana mmoja aliyemshinda Ayubu, Wala kumjibu maneno yake, kati yenu.

Ayabu 32:13 Job 32:13

Jitunzeni msiseme, Sisi tumepata hekima; Mungu yumkini akamshinda, si mtu;

Ayabu 32:14 Job 32:14

Kwa kuwa yeye hajayaelekeza maneno yake kwangu; Wala sitamjibu mimi kwa maneno yenu.

Ayabu 32:15 Job 32:15

Wameshangaa, hawajibu tena; Hawana neno la kusema.

Ayabu 32:16 Job 32:16

Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni, Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena;

Ayabu 32:17 Job 32:17

Mimi nami nitajibu sehemu yangu, Mimi nami nitaonyesha nionavyo.

Ayabu 32:18 Job 32:18

Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.

Ayabu 32:19 Job 32:19

Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; Kama viriba vipya li karibu na kupasuka.

Ayabu 32:20 Job 32:20

Nitanena, ili nipate kutulia; Nitafunua midomo yangu na kujibu.

Ayabu 32:21 Job 32:21

Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu; Wala sitajipendekeza kwa mtu ye yote.

Ayabu 32:22 Job 32:22

Kwani mimi sijui kujipendekeza; Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.