Ayabu Mlango 16 Job

Ayabu 16:1 Job 16:1

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

Ayabu 16:2 Job 16:2

Nimesikia maneno mengi mfano wa hayo; Ninyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha.

Ayabu 16:3 Job 16:3

Je! Maneno yasiyo faida yatakuwa na mwisho? Au, kuna nini kinachokukasirisha, hata ukajibu?

Ayabu 16:4 Job 16:4

Mimi nami ningeweza kunena kama ninyi; Kama roho zenu zingekuwa mahali pa roho yangu, Ningeweza kutunga maneno juu yenu, Na kuwatikisia ninyi kichwa changu.

Ayabu 16:5 Job 16:5

Lakini ningewatia nguvu kwa kinywa changu, Na utuzo wa midomo yangu ungetuliza.

Ayabu 16:6 Job 16:6

Nijapokuwa nanena, huzuni yangu haitulizwi; Nijapokuwa najizuia, nimepunguziwa kitu gani?

Ayabu 16:7 Job 16:7

Lakini sasa amenichokesha; Jamii yangu yote umeifanya ukiwa.

Ayabu 16:8 Job 16:8

Umenishika sana, ni ushahidi juu yangu; Na kukonda kwangu kwaniinukia, kwanishuhudia usoni pangu.

Ayabu 16:9 Job 16:9

Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesaga-saga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali.

Ayabu 16:10 Job 16:10

Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hujikutanisha pamoja juu yangu.

Ayabu 16:11 Job 16:11

Mungu amenitia kwa hao wapotovu, Na kunitupa mikononi mwao waovu.

Ayabu 16:12 Job 16:12

Nilikuwa katika raha, naye akanivunja-vunja; Naam, amenishika shingo, na kuniponda; Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.

Ayabu 16:13 Job 16:13

Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote, Hunipasua viuno vyangu, asinihurumie; Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.

Ayabu 16:14 Job 16:14

Hunivunja kwa uvunjifu juu ya uvunjifu; Hunishambulia mfano wa jitu shujaa.

Ayabu 16:15 Job 16:15

Nimeshona nguo ya magunia juu ya mwili wangu, Na pembe yangu nimeidhili uvumbini.

Ayabu 16:16 Job 16:16

Uso wangu umeharibika kwa kutoa machozi, Na giza tupu li katika kope zangu;

Ayabu 16:17 Job 16:17

Ijapokuwa hapana jeuri mikononi mwangu, Na kuomba kwangu ni safi.

Ayabu 16:18 Job 16:18

Ee nchi, usiifunike damu yangu, Na kilio changu kisipate mahali pa kupumzika.

Ayabu 16:19 Job 16:19

Hata sasa, tazama, shahidi wangu yuko mbinguni. Na huyo atakayenidhamini yuko juu.

Ayabu 16:20 Job 16:20

Rafiki zangu hunidharau; Lakini jicho langu humwagia Mungu machozi;

Ayabu 16:21 Job 16:21

Laiti angemtolea mtu hoja mbele ya Mungu, Amtetee na mwanadamu mbele ya jirani yake.

Ayabu 16:22 Job 16:22

Kwani ikiisha pita miaka michache, Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.