Ayabu Mlango 41 Job

Ayabu 41:1 Job 41:1

Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?

Ayabu 41:2 Job 41:2

Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu?

Ayabu 41:3 Job 41:3

Je! Atakusihi sana? Au, atakuambia maneno ya upole?

Ayabu 41:4 Job 41:4

Je! Atafanya agano pamoja nawe, Umtwae kuwa mtumishi wako milele?

Ayabu 41:5 Job 41:5

Je! Utamchezea kama ndege? Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako?

Ayabu 41:6 Job 41:6

Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara? Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?

Ayabu 41:7 Job 41:7

Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha, Au kichwa chake kwa vyusa?

Ayabu 41:8 Job 41:8

Mwekee mkono wako; Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena.

Ayabu 41:9 Job 41:9

Tazama, kumtamani ni bure; Je! Hatambwaga chini huyo atakayemtazama?

Ayabu 41:10 Job 41:10

Hapana aliye mkali hata akathubutu kumwamsha; Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi?

Ayabu 41:11 Job 41:11

Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.

Ayabu 41:12 Job 41:12

Sitanyamaa kusema habari za via vyake, Wala nguvu zake kuu, wala umbo lake zuri.

Ayabu 41:13 Job 41:13

Ni nani awezaye kumbambua magamba yake? Ni nani atakayepenya dirii yake maradufu?

Ayabu 41:14 Job 41:14

Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake? Meno yake yatisha kandokando yake.

Ayabu 41:15 Job 41:15

Magamba yake yenye nguvu ndiyo fahari yake, Yamefungamana pamoja kama kwa kufungwa kwa muhuri.

Ayabu 41:16 Job 41:16

Jinsi yalivyoshikamana Hata upepo hauwezi kupita kati.

Ayabu 41:17 Job 41:17

Yamefungamana pamoja; Yameshikamana, hata hayawezekani kutengwa.

Ayabu 41:18 Job 41:18

Kwa kuchemua kwake mwanga humemetuka, Na macho yake yanafanana na makope ya alfajiri.

Ayabu 41:19 Job 41:19

Mienge iwakayo hutoka kinywani mwake, Na macheche ya moto huruka nje.

Ayabu 41:20 Job 41:20

Moshi hutoka katika mianzi ya pua yake, Kama nyungu ikitokota, na manyasi yawakayo.

Ayabu 41:21 Job 41:21

Pumzi zake huwasha makaa, Na miali ya moto hutoka kinywani mwake.

Ayabu 41:22 Job 41:22

Katika shingo yake hukaa nguvu, Na utisho hucheza mbele yake.

Ayabu 41:23 Job 41:23

Manofu ya nyama yake hushikamana; Yanakazana juu yake; hayawezi kuondolewa.

Ayabu 41:24 Job 41:24

Moyo wake una imara kama jiwe; Naam, imara kama jiwe la chini la kusagia.

Ayabu 41:25 Job 41:25

Anapojiinua, mashujaa huogopa; Kwa sababu ya woga wao huvunjwa moyo.

Ayabu 41:26 Job 41:26

Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii; Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.

Ayabu 41:27 Job 41:27

Yeye huona chuma kuwa kama nyasi, Na shaba kama mti uliooza.

Ayabu 41:28 Job 41:28

Mshale hauwezi kumkimbiza; Na mawe ya teo kwake hugeuka kuwa kama makapi.

Ayabu 41:29 Job 41:29

Marungu huhesabiwa kama mabua; Naye hucheka mshindo wa mkuki ukitupwa.

Ayabu 41:30 Job 41:30

Pande zake za chini ni kama vigae vikali; Hutandika malazi kama kuweka chombo cha kupuria nafaka juu ya matope.

Ayabu 41:31 Job 41:31

Yeye huchemsha kilindi mfano wa nyungu; Hufanya bahari kuwa kama mafuta.

Ayabu 41:32 Job 41:32

Hufanya mapito yake kung'aa nyuma yake Hata mtu angedhani kilindi kina mvi.

Ayabu 41:33 Job 41:33

Juu ya nchi hapana aliyefanana naye, Aliyeumbwa pasipo oga.

Ayabu 41:34 Job 41:34

Yeye hutazama kila kitu kilicho juu; Ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.