Ayabu Mlango 27 Job

Ayabu 27:1 Job 27:1

Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema,

Ayabu 27:2 Job 27:2

Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu; Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu;

Ayabu 27:3 Job 27:3

(Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu, Na roho ya Mungu i katika pua yangu;)

Ayabu 27:4 Job 27:4

Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki, Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.

Ayabu 27:5 Job 27:5

Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki; Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu.

Ayabu 27:6 Job 27:6

Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha; Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.

Ayabu 27:7 Job 27:7

Adui yangu na awe kama huyo mwovu, Na mwenye kuondoka kinyume changu na awe kama asiye haki.

Ayabu 27:8 Job 27:8

Kwani tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida, Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?

Ayabu 27:9 Job 27:9

Je! Mungu atakisikia kilio chake, Taabu zitakapomfikilia?

Ayabu 27:10 Job 27:10

Je! Atajifurahisha katika Mwenyezi, Na kumlingana Mungu nyakati zote?

Ayabu 27:11 Job 27:11

Nitawafundisha ninyi mambo ya mkono wa Mungu; Hayo yaliyo kwa Mwenyezi sitayaficha.

Ayabu 27:12 Job 27:12

Tazama, ninyi nyote mmeyaona wenyewe; Mbona basi mmebatilika kabisa?

Ayabu 27:13 Job 27:13

Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu, Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi.

Ayabu 27:14 Job 27:14

Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga; Na wazao wake hawatashiba chakula.

Ayabu 27:15 Job 27:15

Hao watakaosalia kwake watazikwa katika kufa, Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza.

Ayabu 27:16 Job 27:16

Ajapokusanya fedha kama mavumbi, Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi;

Ayabu 27:17 Job 27:17

Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa, Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha.

Ayabu 27:18 Job 27:18

Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu, Na kama kibanda afanyacho mlinzi.

Ayabu 27:19 Job 27:19

Yeye hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho; Hufunua macho yake, naye hayuko.

Ayabu 27:20 Job 27:20

Vitisho vyampata kama maji mengi; Dhoruba humwiba usiku.

Ayabu 27:21 Job 27:21

Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka; Na kumkumba atoke mahali pake.

Ayabu 27:22 Job 27:22

Kwani Mungu atamtupia asimhurumie; Angependa kuukimbia mkono wake.

Ayabu 27:23 Job 27:23

Watu watampigia makofi, Na kumzomea atoke mahali pake.