Ayabu Mlango 34 Job

Ayabu 34:1 Job 34:1

Tena Elihu akajibu na kusema,

Ayabu 34:2 Job 34:2

Sikilizeni maneno yangu, enyi wenye hekima; Tegeni masikio kwangu, ninyi mlio na maarifa.

Ayabu 34:3 Job 34:3

Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno, Kama vile kaakaa lionjavyo chakula.

Ayabu 34:4 Job 34:4

Na tujichagulie yaliyo ya uelekevu; Na tujue wenyewe yaliyo mema.

Ayabu 34:5 Job 34:5

Kwani Ayubu amesema, Mimi ni mwenye haki, Naye Mungu ameniondolea haki yangu;

Ayabu 34:6 Job 34:6

Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo; Jeraha yangu haiponyeki, nijapokuwa sina makosa.

Ayabu 34:7 Job 34:7

Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu, Anywaye mzaha kama maji?

Ayabu 34:8 Job 34:8

Atembeaye na hao watendao uovu, Na kwenda pamoja na watu wabaya.

Ayabu 34:9 Job 34:9

Kwa kuwa amenena, Haimfai mtu lo lote Kujifurahisha na Mungu.

Ayabu 34:10 Job 34:10

Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye fahamu; Mungu asidhaniwe kutenda udhalimu; Wala Mwenyezi kufanya uovu.

Ayabu 34:11 Job 34:11

Kwani atamlipa binadamu kwa kazi yake, Naye atamfanya kila mtu kuona sawasawa na njia zake

Ayabu 34:12 Job 34:12

Naam, hakika, Mungu hatatenda mabaya, Wala Mwenyezi hatapotosha hukumu.

Ayabu 34:13 Job 34:13

Ni nani aliyemwagiza kuiangalia dunia? Au ni nani aliyemwekea ulimwengu huu wote?

Ayabu 34:14 Job 34:14

Kama akimwekea mtu moyo wake, Akijikusanyia roho yake na pumzi zake;

Ayabu 34:15 Job 34:15

Wenye mwili wote wataangamia pamoja, Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.

Ayabu 34:16 Job 34:16

Ikiwa una ufahamu, sikia neno hili; Isikilize sauti ya maneno yangu.

Ayabu 34:17 Job 34:17

Je! Atatawala mtu aichukiaye haki hata mmoja? Nawe, je! Utamhukumia mkosa aliye na haki na mwenye nguvu?

Ayabu 34:18 Job 34:18

Je! Inafaa kumwambia mfalme, Wewe u mwovu? Au kuwaambia wakuu, Ninyi ni wabaya?

Ayabu 34:19 Job 34:19

Sembuse huyo asiyependelea nyuso za wakuu, Wala hawajali matajiri kuliko maskini? Kwani wote ni kazi ya mikono yake,

Ayabu 34:20 Job 34:20

Hufa ghafula, hata usiku wa manane; Watu hutikisika na kwenda zao, Nao mashujaa huondolewa pasipo mkono wa mtu.

Ayabu 34:21 Job 34:21

Kwani macho yake ya juu ya njia za mtu, Naye huiona miendo yake yote.

Ayabu 34:22 Job 34:22

Hapana weusi, wala hilo giza tupu, Wawezapo kujificha watendao udhalimu.

Ayabu 34:23 Job 34:23

Kwani yeye hana haja ya kumfikiria mtu zaidi, ili aende mbele za Mungu ahukumiwe.

Ayabu 34:24 Job 34:24

Yeye huwavunja-vunja mashujaa pasina kuwachunguza, Na kuwaweka wengine mahali pao.

Ayabu 34:25 Job 34:25

Kwa sababu hiyo yeye huyatafiti matendo yao; Naye huwapindia usiku, wakaangamia.

Ayabu 34:26 Job 34:26

Yeye huwapiga kama watu wabaya Waziwazi mbele ya macho ya wengine;

Ayabu 34:27 Job 34:27

Kwa sababu walikengeuka, wasimwandame yeye, Wasikubali kuzishika njia zake hata moja;

Ayabu 34:28 Job 34:28

Hata wakafanya kilio cha maskini kumfikilia, Naye akasikia kilio cha hao wateswao.

Ayabu 34:29 Job 34:29

Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;

Ayabu 34:30 Job 34:30

Kwamba huyo mpotovu asitawale, Pasiwe na wa kuwatega watu.

Ayabu 34:31 Job 34:31

Kwani kuna mtu aliyemwambia Mungu, Mimi nimevumilia kurudiwa, ingawa sikukosa;

Ayabu 34:32 Job 34:32

Nisiyoyaona nifundishe wewe; Kama nimefanya uovu sitafanya tena?

Ayabu 34:33 Job 34:33

Je! Malipo yake yatakuwa kama upendavyo wewe, hata ukayakataa? Kwani yakupasa wewe kuchagua, si mimi; Kwa sababu hiyo sema uyajuayo.

Ayabu 34:34 Job 34:34

Watu walio na akili wataniambia, Naam, kila mtu mwenye hekima anisikiaye;

Ayabu 34:35 Job 34:35

Huyo Ayubu amesema pasipo maarifa, Na maneno yake hayana hekima.

Ayabu 34:36 Job 34:36

Laiti Ayubu angejaribiwa hata mwisho, Kwa kuwa amejibu kama watu waovu.

Ayabu 34:37 Job 34:37

Kwani huongeza uasi juu ya dhambi zake, Apiga makofi kati yetu, Na kuongeza maneno yake kinyume cha Mungu.