Ayabu Mlango 38 Job

Ayabu 38:1 Job 38:1

Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,

Ayabu 38:2 Job 38:2

Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa?

Ayabu 38:3 Job 38:3

Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie.

Ayabu 38:4 Job 38:4

Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.

Ayabu 38:5 Job 38:5

Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?

Ayabu 38:6 Job 38:6

Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,

Ayabu 38:7 Job 38:7

Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?

Ayabu 38:8 Job 38:8

Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni.

Ayabu 38:9 Job 38:9

Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,

Ayabu 38:10 Job 38:10

Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango,

Ayabu 38:11 Job 38:11

Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa?

Ayabu 38:12 Job 38:12

Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?

Ayabu 38:13 Job 38:13

Yapate kuishika miisho ya nchi, Waovu wakung'utwe wakawe mbali nayo?

Ayabu 38:14 Job 38:14

Hubadilika mfano wa udongo chini ya muhuri, Vitu vyote vinatokea kama mavazi.

Ayabu 38:15 Job 38:15

Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, Na mkono ulioinuka huvunjika.

Ayabu 38:16 Job 38:16

Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi?

Ayabu 38:17 Job 38:17

Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?

Ayabu 38:18 Job 38:18

Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.

Ayabu 38:19 Job 38:19

Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi?

Ayabu 38:20 Job 38:20

Upate kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake?

Ayabu 38:21 Job 38:21

Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, Na hesabu ya siku zako ni kubwa!

Ayabu 38:22 Job 38:22

Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe,

Ayabu 38:23 Job 38:23

Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita?

Ayabu 38:24 Job 38:24

Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi?

Ayabu 38:25 Job 38:25

Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika, Au njia kwa umeme wa radi;

Ayabu 38:26 Job 38:26

Kunyesha mvua juu ya nchi isiyo na watu; Juu ya jangwa asiyokaa mwanadamu;

Ayabu 38:27 Job 38:27

Kuishibisha nchi iliyo kame na ukiwa, Na kuyameza majani yaliyo mororo?

Ayabu 38:28 Job 38:28

Je! Mvua ina baba? Au ni nani aliyeyazaa matone ya umande?

Ayabu 38:29 Job 38:29

Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa?

Ayabu 38:30 Job 38:30

Maji hugandamana kama jiwe, Na uso wa vilindi huganda kwa baridi.

Ayabu 38:31 Job 38:31

Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia, Au kuvilegeza vifungo vya Orioni?

Ayabu 38:32 Job 38:32

Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake?

Ayabu 38:33 Job 38:33

Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?

Ayabu 38:34 Job 38:34

Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, ili wingi wa maji ukufunikize?

Ayabu 38:35 Job 38:35

Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda, Ukakuambia, Sisi tupo hapa?

Ayabu 38:36 Job 38:36

Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni? Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni?

Ayabu 38:37 Job 38:37

Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu kwa hekima? Au ni nani awezaye kuzimimina chupa za mbinguni?

Ayabu 38:38 Job 38:38

Wakati mavumbi yagandamanapo, Na madongoa kushikamana pamoja?

Ayabu 38:39 Job 38:39

Je! Utamwindia simba mke mawindo? Au utashibisha njaa ya simba wachanga,

Ayabu 38:40 Job 38:40

Waoteapo mapangoni mwao, Wakaapo mafichoni wapate kuvizia?

Ayabu 38:41 Job 38:41

Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutanga-tanga kwa kutindikiwa na chakula?