Ayabu Mlango 3 Job

Ayabu 3:1 Job 3:1

Baada ya hayo Ayubu akafunua kinywa chake, na kuilaani siku yake.

Ayabu 3:2 Job 3:2

Ayubu akajibu, na kusema;

Ayabu 3:3 Job 3:3

Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, Na ule usiku uliosema, Mtoto mume ametungishwa mimba.

Ayabu 3:4 Job 3:4

Siku hiyo na iwe giza; Mungu asiiangalie toka juu, Wala mwanga usiiangazie.

Ayabu 3:5 Job 3:5

Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake; Wingu na likae juu yake; Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe.

Ayabu 3:6 Job 3:6

Tena usiku huo, na ushikwe na giza kuu; Usihesabiwe katika siku za mwaka; Wala kutiwa katika hesabu ya miezi.

Ayabu 3:7 Job 3:7

Tazama, usiku huo na uwe tasa; Wala isiwe ndani yake sauti ya shangwe.

Ayabu 3:8 Job 3:8

Na waulaani hao waulaanio mchana, Hao walio tayari kumwamsha huyo lewiathani.

Ayabu 3:9 Job 3:9

Nyota za mapambazuko yake na ziwe giza; Na utafute mwanga lakini usiupate; Wala usiyaone makope ya asubuhi;

Ayabu 3:10 Job 3:10

Kwa sababu haukuifunga milango ya tumbo la mamangu. Wala kunifichia taabu machoni.

Ayabu 3:11 Job 3:11

Mbona si kufa mimi tokea mimbani? Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni?

Ayabu 3:12 Job 3:12

Mbona hayo magoti kunipokea? Au hayo maziwa, hata nikanyonya?

Ayabu 3:13 Job 3:13

Maana hapo ningelala na kutulia; Ningelala usingizi; na kupata kupumzika;

Ayabu 3:14 Job 3:14

Pamoja na wafalme na washauri wa dunia, Hao waliojijengea maganjoni;

Ayabu 3:15 Job 3:15

Au pamoja na wakuu wenye dhahabu, Waliozijaza fedha nyumba zao;

Ayabu 3:16 Job 3:16

Au, kama kuzikwa mimba iliyoharibika, nisingekuwako; Kama wachanga wasiouona mwanga kabisa.

Ayabu 3:17 Job 3:17

Huko waovu huacha kusumbua; Huko nako hao waliochoka wapumzika

Ayabu 3:18 Job 3:18

Huko wafungwa waona raha pamoja; Hawaisikii sauti yake msimamizi.

Ayabu 3:19 Job 3:19

Wakuu na wadogo wako huko; Mtumishi yu huru kwa bwana wake.

Ayabu 3:20 Job 3:20

Mbona yeye aliye mashakani kupewa mwanga, Na hao wenye uchungu rohoni kupewa uhai;

Ayabu 3:21 Job 3:21

Ambao wangojea mauti, lakini hawayapati; Na kuyachimbulia zaidi ya kutafuta hazina iliyostirika;

Ayabu 3:22 Job 3:22

Ambao wafurahi mno, Na kushangilia watakapoliona kaburi?

Ayabu 3:23 Job 3:23

Kwa nini mtu aliyezibiwa njia kupewa mwanga, Ambaye Mungu amemzingira kwa ukingo?

Ayabu 3:24 Job 3:24

Kwani kuugua kwangu kwaja kana kwamba ni chakula, Na kunguruma kwangu kumemiminika kama maji.

Ayabu 3:25 Job 3:25

Maana jambo hilo nichalo hunipata, Nalo linitialo hofu hunijilia.

Ayabu 3:26 Job 3:26

Mimi sioni raha, wala situlii, wala kupumzika; Lakini huja taabu.