Ayabu Mlango 18 Job

Ayabu 18:1 Job 18:1

Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,

Ayabu 18:2 Job 18:2

Je! Hata lini utayategea maneno mitambo? Fikiri, kisha baadaye tutanena.

Ayabu 18:3 Job 18:3

Twahesabiwa kuwa wanyama kwa sababu gani, Tena kuwa wanajisi machoni pako?

Ayabu 18:4 Job 18:4

Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako, Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe? Au jabali litaondolewa mahali pake?

Ayabu 18:5 Job 18:5

Naam, mwanga wa waovu utazimika, Wala mwali wa moto wake hautang'aa.

Ayabu 18:6 Job 18:6

Mwanga hemani mwake utakuwa giza, Nayo taa iliyo juu yake itazimishwa.

Ayabu 18:7 Job 18:7

Hatua zake za nguvu zitasongwa, Na shauri lake mwenyewe litamwangusha chini.

Ayabu 18:8 Job 18:8

Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe, Naye huenda juu ya matanzi.

Ayabu 18:9 Job 18:9

Tanzi litamshika kisigino chake, Na mtambo utamgwia.

Ayabu 18:10 Job 18:10

Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani.

Ayabu 18:11 Job 18:11

Matisho yatamtia hofu pande zote, Na kumfukuza karibu na visigino vyake.

Ayabu 18:12 Job 18:12

Nguvu zake zitaliwa na njaa, Na msiba utakuwa tayari kwa kusita kwake.

Ayabu 18:13 Job 18:13

Utakula via vya mwili wake, Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake.

Ayabu 18:14 Job 18:14

Atang'olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa kwake mfalme wa utisho.

Ayabu 18:15 Job 18:15

Ambacho si chake kitakaa katika hema yake; Kiberiti kitamwagwa juu ya makazi yake.

Ayabu 18:16 Job 18:16

Chini, mizizi yake itakaushwa; Na juu, tawi lake litasinyaa.

Ayabu 18:17 Job 18:17

Kumbukumbu lake litakoma katika nchi, Wala hatakuwa na jina mashambani.

Ayabu 18:18 Job 18:18

Atakimbizwa kutoka mwangani hata gizani, Na kufukuzwa atoke duniani.

Ayabu 18:19 Job 18:19

Hatakuwa na mwana wala mjukuu kati ya watu wake, Wala hatasalia mtu hapo alipokaa.

Ayabu 18:20 Job 18:20

Hao wanaokaa magharibi watastaajabia siku yake, Kama vile wanaokaa mashariki walivyotiwa hofu.

Ayabu 18:21 Job 18:21

Hakika ndivyo yalivyo makazi ya wapotovu, Na hapa ni mahali pake asiyemjua Mungu.