Ayabu Mlango 9 Job

Ayabu 9:1 Job 9:1

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

Ayabu 9:2 Job 9:2

Kweli najua kuwa ndivyo hivyo; Lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu?

Ayabu 9:3 Job 9:3

Kama akipenda kushindana naye, Hawezi kumjibu neno moja katika elfu.

Ayabu 9:4 Job 9:4

Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?

Ayabu 9:5 Job 9:5

Aiondoaye milima, nayo haina habari, Akiipindua katika hasira zake.

Ayabu 9:6 Job 9:6

Aitikisaye dunia itoke mahali pake, Na nguzo zake hutetema.

Ayabu 9:7 Job 9:7

Aliamuruye jua, nalo halichomozi; Nazo nyota huzipiga muhuri.

Ayabu 9:8 Job 9:8

Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu, Na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.

Ayabu 9:9 Job 9:9

Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hicho Kilimia, Na makundi ya nyota ya kusini.

Ayabu 9:10 Job 9:10

Atendaye mambo makuu yasiyotafutikana; Naam, mambo ya ajabu yasiyohesabika.

Ayabu 9:11 Job 9:11

Tazama, yuaenenda karibu nami, nisimwone; Tena yuapita kwenda mbele, nisimtambue.

Ayabu 9:12 Job 9:12

Tazama, yuakamata, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwuliza, Wafanya nini?

Ayabu 9:13 Job 9:13

Mungu haondoi hasira zake; Hao wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.

Ayabu 9:14 Job 9:14

Je! Mimi nitamjibuje, Na kuyachagua maneno yangu kuhojiana naye?

Ayabu 9:15 Job 9:15

Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, nisingemjibu; Ningemsihi-sihi mtesi wangu.

Ayabu 9:16 Job 9:16

Kama ningemwita, naye akaniitikia; Hata hivyo singeamini kuwa amesikiza sauti yangu.

Ayabu 9:17 Job 9:17

Yeye anipondaye kwa dhoruba, Na kuziongeza jeraha zangu pasipokuwa na sababu.

Ayabu 9:18 Job 9:18

Haniachi nipate kuvuta pumzi, Lakini hunijaza uchungu.

Ayabu 9:19 Job 9:19

Kama tukitaja nguvu za mashujaa, tazama yupo hapo! Kama tukitaja hukumu, ni nani atakayeniwekea muhula?

Ayabu 9:20 Job 9:20

Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; Ingawa ni mkamilifu, kitanishuhudia kuwa ni mpotovu.

Ayabu 9:21 Job 9:21

Mimi ni mkamilifu; siangalii nafsi yangu; Naudharau uhai wangu.

Ayabu 9:22 Job 9:22

Hayo yote ni mamoja; kwa hiyo nasema, Yeye huangamiza wakamilifu na waovu pia.

Ayabu 9:23 Job 9:23

Kama hilo pigo likiua ghafula, Atayadhihaki majaribu yake asiye na kosa.

Ayabu 9:24 Job 9:24

Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?

Ayabu 9:25 Job 9:25

Basi siku zangu zina mbio kuliko tarishi; Zakimbia, wala hazioni mema.

Ayabu 9:26 Job 9:26

Zimepita kama merikebu ziendazo mbio; Mfano wa tai ayashukiaye mawindo.

Ayabu 9:27 Job 9:27

Nikisema, Mimi nitasahau kuugua kwangu, Nitaacha kununa uso nikachangamke moyo;

Ayabu 9:28 Job 9:28

Mimi huziogopa huzuni zangu zote, Najua kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia.

Ayabu 9:29 Job 9:29

Nitahukumiwa kuwa ni mkosa; Ya nini basi nitaabike bure?

Ayabu 9:30 Job 9:30

Ingawaje najiosha kwa maji ya theluji, Na kuitakasa mikono yangu kwa sabuni;

Ayabu 9:31 Job 9:31

Lakini utanitupa shimoni, Nami hata nguo zangu zitanichukia.

Ayabu 9:32 Job 9:32

Kwani yeye si mtu, kama mimi, hata nimjibu, Hata tukaribiane katika hukumu.

Ayabu 9:33 Job 9:33

Hapana mwenye kuamua katikati yetu, Awezaye kutuwekea mkono sote wawili.

Ayabu 9:34 Job 9:34

Na aniondolee fimbo yake, Na utisho wake usinitie hofu;

Ayabu 9:35 Job 9:35

Ndipo hapo ningesema, nisimwogope; Kwani sivyo nilivyo nafsini mwangu.