Ayabu Mlango 25 Job

Ayabu 25:1 Job 25:1

Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,

Ayabu 25:2 Job 25:2

Enzi na hofu zi pamoja naye; Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.

Ayabu 25:3 Job 25:3

Je! Majeshi yake yahesabika? Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?

Ayabu 25:4 Job 25:4

Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?

Ayabu 25:5 Job 25:5

Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake;

Ayabu 25:6 Job 25:6

Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!