Ayabu Mlango 28 Job

Ayabu 28:1 Job 28:1

Hakika kuna shimo wachimbako fedha, Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo.

Ayabu 28:2 Job 28:2

Chuma hufukuliwa katika ardhi, Na shaba huyeyushwa katika mawe.

Ayabu 28:3 Job 28:3

Binadamu hukomesha giza; Huyatafuta-tafuta hata mpaka ulio mbali, Mawe ya giza kuu, giza tupu.

Ayabu 28:4 Job 28:4

Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning'inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko.

Ayabu 28:5 Job 28:5

Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula; Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto.

Ayabu 28:6 Job 28:6

Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti; Nayo ina mchanga wa dhahabu.

Ayabu 28:7 Job 28:7

Njia ile hapana ndege mkali aijuaye, Wala jicho la tai halijaiona;

Ayabu 28:8 Job 28:8

Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga, Wala simba mkali hajaipita.

Ayabu 28:9 Job 28:9

Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake.

Ayabu 28:10 Job 28:10

Hukata mifereji kati ya majabali; Na jicho lake huona kila kito cha thamani

Ayabu 28:11 Job 28:11

Hufunga vijito visichuruzike; Na kitu kilichostirika hukifunua.

Ayabu 28:12 Job 28:12

Bali hekima itapatikana wapi? Na mahali pa ufahamu ni wapi?

Ayabu 28:13 Job 28:13

Mwanadamu hajui thamani yake, Wala haionekani katika nchi ya walio hai.

Ayabu 28:14 Job 28:14

Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu; Na bahari yasema, Haiko kwangu.

Ayabu 28:15 Job 28:15

Haipatikani kwa dhahabu, Wala fedha haitapimwa iwe thamani yake.

Ayabu 28:16 Job 28:16

Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti ya samawi.

Ayabu 28:17 Job 28:17

Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi.

Ayabu 28:18 Job 28:18

Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani.

Ayabu 28:19 Job 28:19

Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo, Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi.

Ayabu 28:20 Job 28:20

Basi hekima yatoka wapi? Na mahali pa ufahamu ni wapi?

Ayabu 28:21 Job 28:21

Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai, Na kusitirika na ndege wa angani.

Ayabu 28:22 Job 28:22

Uharibifu na Mauti husema, Tumesikia habari zake kwa masikio yetu.

Ayabu 28:23 Job 28:23

Mungu ndiye aijuaye njia yake, Naye anajua mahali pake.

Ayabu 28:24 Job 28:24

Maana anatazama hata miisho ya nchi, Na kuona chini ya mbingu nzima.

Ayabu 28:25 Job 28:25

Apate kuufanyia upepo uzito wake; Naam, anayapima maji kwa kipimo.

Ayabu 28:26 Job 28:26

Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa umeme wa radi.

Ayabu 28:27 Job 28:27

Ndipo alipoiona na kuitangaza; Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.

Ayabu 28:28 Job 28:28

Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.