Ayabu Mlango 35 Job

Ayabu 35:1 Job 35:1

Tena Elihu akajibu na kusema,

Ayabu 35:2 Job 35:2

Je! Wewe wadhani kwamba haya ni haki yako, Au je! Wasema, Haki yangu ni zaidi kuliko ya Mungu,

Ayabu 35:3 Job 35:3

Maana wasema, Kutakuwa na faida gani kwako wewe? Tena, Nitapata faida gani, kuliko nikifanya dhambi?

Ayabu 35:4 Job 35:4

Mimi nitakujibu, Na hawa wenzio pamoja nawe.

Ayabu 35:5 Job 35:5

Ziangalie mbingu ukaone; Na mawingu yaangalie, yaliyo juu kuliko wewe.

Ayabu 35:6 Job 35:6

Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?

Ayabu 35:7 Job 35:7

Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani? Au yeye hupokea nini mkononi mwako?

Ayabu 35:8 Job 35:8

Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe; Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu.

Ayabu 35:9 Job 35:9

Kwa sababu ya wingi wa jeuri wao hulia; Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu.

Ayabu 35:10 Job 35:10

Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu, Awapaye nyimbo wakati wa usiku;

Ayabu 35:11 Job 35:11

Atufundishaye zaidi ya hayawani wa nchi, Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege za angani?

Ayabu 35:12 Job 35:12

Hulia huko, lakini hapana ajibuye, Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.

Ayabu 35:13 Job 35:13

Hakika Mungu hatasikia ubatili, Wala Mwenyezi hatauangalia.

Ayabu 35:14 Job 35:14

Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii, Hiyo daawa i mbele yake, nawe wamngojea!

Ayabu 35:15 Job 35:15

Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujilia katika hasira zake, Wala hauangalii sana unyeti;

Ayabu 35:16 Job 35:16

Ndiposa Ayubu hufunua kinywa chake kwa ubatili; Huongeza maneno pasipo maarifa.