Ayabu Mlango 39 Job

Ayabu 39:1 Job 39:1

Je! Wajua majira ya kuzaa kwao mbuzi-mwitu walio majabalini? Au waweza kusema majira ya kuzaa kulungu?

Ayabu 39:2 Job 39:2

Je! Waweza kuhesabu miezi yao watakayoitimiza? Au je! Wajua majira ya kuzaa kwao?

Ayabu 39:3 Job 39:3

Wao hujiinamisha, kuzaa watoto wao, Watupa taabu zao.

Ayabu 39:4 Job 39:4

Watoto wao wa katika hali nzuri, hukua katika bara wazi; Huenda zao, wala hawarudi tena.

Ayabu 39:5 Job 39:5

Ni nani aliyempeleka punda-milia aende huru? Au je! Ni nani aliyemfungulia vifungo punda-mwitu?

Ayabu 39:6 Job 39:6

Ambaye nimeifanya nyika kuwa nyumba yake, Na nchi ya chumvi kuwa makao yake.

Ayabu 39:7 Job 39:7

Yeye hudharau mshindo wa mji, Wala hasikii kelele zake msimamizi.

Ayabu 39:8 Job 39:8

Upana wa milima ni malisho yake, Hutafuta-tafuta kila kitu kilicho kibichi.

Ayabu 39:9 Job 39:9

Je! Nyati atakubali kukutumikia? Au atakaa katika zizi lako?

Ayabu 39:10 Job 39:10

Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani? Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako?

Ayabu 39:11 Job 39:11

Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi? Au, utamwachia yeye kazi yako?

Ayabu 39:12 Job 39:12

Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani. Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria?

Ayabu 39:13 Job 39:13

Bawa la mbuni hufurahi; Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma?

Ayabu 39:14 Job 39:14

Kwani yeye huyaacha mayai yake juu ya nchi, Na kuyatia moto mchangani,

Ayabu 39:15 Job 39:15

Na kusahau kwamba yumkini mguu kuyavunja, Au mnyama wa mwitu kuyakanyaga.

Ayabu 39:16 Job 39:16

yeye huyafanyia ukali makinda yake, kana kwamba si yake; Ijapokuwa taabu yake ni ya bure, hana hofu;

Ayabu 39:17 Job 39:17

Kwa sababu Mungu amemnyima akili, Wala hakumpa fahamu.

Ayabu 39:18 Job 39:18

Wakati anapojiinua juu aende, Humdharau farasi na mwenye kumpanda.

Ayabu 39:19 Job 39:19

Je! Wewe ulimpa farasi uwezo wake? Au, ni wewe uliyemvika shingo yake manyoya yatetemayo?

Ayabu 39:20 Job 39:20

Ndiwe uliyemfanya aruke kama nzige? Fahari ya mlio wake hutisha.

Ayabu 39:21 Job 39:21

Hupara-para bondeni, na kuzifurahia nguvu zake; Hutoka kwenda kukutana na wenye silaha.

Ayabu 39:22 Job 39:22

Yeye hufanyia kicho dhihaka, wala hashangai; Wala hageuki kurudi nyuma mbele ya upanga.

Ayabu 39:23 Job 39:23

Podo humpigia makelele, Mkuki ung'aao na fumo.

Ayabu 39:24 Job 39:24

Huimeza nchi kwa ukali wake na ghadhabu; Wala hasimami kwa sauti ya baragumu.

Ayabu 39:25 Job 39:25

Kila ipigwapo baragumu yeye husema, Aha! Naye husikia harufu ya vita toka mbali, Mshindo wa maakida, na makelele.

Ayabu 39:26 Job 39:26

Je! Mwewe huruka juu kwa akili zako, Na kuyanyosha mabawa yake kwenda kusini?

Ayabu 39:27 Job 39:27

Je! Tai hupaa juu kwa amri yako, Na kufanya kioto chake mahali pa juu?

Ayabu 39:28 Job 39:28

Hukaa jabalini, ndiko kwenye malazi yake, Juu ya genge la jabali, na ngomeni.

Ayabu 39:29 Job 39:29

Toka huko yeye huchungulia mawindo; Macho yake huyaangalia toka mbali.

Ayabu 39:30 Job 39:30

Makinda yake nayo hufyonza damu; Na kwenye maiti ndiko aliko.