Ayabu Mlango 13 Job

Ayabu 13:1 Job 13:1

Tazama, jicho langu limeyaona hayo yote, Sikio langu limeyasikia na kuelewa nayo.

Ayabu 13:2 Job 13:2

Hayo myajuayo ninyi, na mimi pia nayajua; Mimi si duni kuliko ninyi.

Ayabu 13:3 Job 13:3

Hakika ningenena naye huyo Mwenyezi, Nami nataka kuhojiana na Mungu.

Ayabu 13:4 Job 13:4

Lakini ninyi hubuni maneno ya uongo, Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa.

Ayabu 13:5 Job 13:5

Laiti mngenyamaza kabisa! Hilo lingekuwa hekima kwenu.

Ayabu 13:6 Job 13:6

Sikieni sasa basi hoja zangu, Mkayasikie mashindano ya midomo yangu.

Ayabu 13:7 Job 13:7

Je! Mtanena yasiyo ya haki kwa ajili ya Mungu, Na kusema kwa udanganyifu kwa ajili yake?

Ayabu 13:8 Job 13:8

Je! Mtamwonyesha yeye upendeleo? Mtamtetea Mungu?

Ayabu 13:9 Job 13:9

Je! Itafaa yeye kuwatafuta ninyi? Au, kama kumdanganya mtu, je! Mtamdanganya yeye?

Ayabu 13:10 Job 13:10

Hakika atawakemea ninyi, Mkiwapendelea watu kwa siri.

Ayabu 13:11 Job 13:11

Je! Huo ukuu wake hautawatia hofu, Na utisho wake hautawaangukia?

Ayabu 13:12 Job 13:12

Matamko yenu ya hekima ni mithali ya majivu, Ngome zenu ni ngome za udongo.

Ayabu 13:13 Job 13:13

Nyamazeni, niacheni, ili nipate kunena, Na hayo yatakayonijilia na yaje.

Ayabu 13:14 Job 13:14

Nitaitwaa nyama ya mwili wangu katika meno yangu, Na kuutwaa uhai wangu mkononi mwangu!

Ayabu 13:15 Job 13:15

Tazama, ataniua; sina tumaini; ila hata hivyonitaithibitisha njia yangu mbele yake.

Ayabu 13:16 Job 13:16

Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu; Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake.

Ayabu 13:17 Job 13:17

Sikieni sana maneno yangu, Maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu.

Ayabu 13:18 Job 13:18

Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu, Najua ya kuwa ni mwenye haki mimi.

Ayabu 13:19 Job 13:19

Yuko nani atakayeshindana nami? Maana sasa nitanyamaa kimya na kutoa roho.

Ayabu 13:20 Job 13:20

Lakini msinifanyie mambo mawili, hayo tu, Ndipo nami sitajificha usoni pako;

Ayabu 13:21 Job 13:21

Uondoe mkono wako usinilemee; Na utisho wako usinitie hofu.

Ayabu 13:22 Job 13:22

Basi uite wakati huo, nami nitaitika; Au, niache ninene mimi, nawe unijibu.

Ayabu 13:23 Job 13:23

Maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi? Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.

Ayabu 13:24 Job 13:24

Mbona umeuficha uso wako, Na kunihesabu kuwa ni adui yako?

Ayabu 13:25 Job 13:25

Je! Utalitaabisha jani lipeperushwalo? Au, je! Utayafuatia hayo mabua makavu?

Ayabu 13:26 Job 13:26

Kwani umeandika maneno ya uchungu juu yangu, Na kunirithisha maovu ya ujana wangu;

Ayabu 13:27 Job 13:27

Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyaaua mapito yangu yote; Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu;

Ayabu 13:28 Job 13:28

Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa, Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.