Ayabu Mlango 5 Job

Ayabu 5:1 Job 5:1

Haya, ita sasa; je! Yuko atakayekujibu? Nawe utamwelekea yupi katika hao watakatifu?

Ayabu 5:2 Job 5:2

Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga.

Ayabu 5:3 Job 5:3

Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi; Lakini mara niliyalaani maskani yake.

Ayabu 5:4 Job 5:4

Watoto wake wako mbali na wokovu, Nao wamesongwa langoni, Wala hapana atakayewaponya.

Ayabu 5:5 Job 5:5

Mavuno yake wale wenye njaa huyala, Na kuyatwaa hata kuyatoa miibani, Nao wenye kiu huzitwetea mali zao.

Ayabu 5:6 Job 5:6

Kwani taabu haitoki mchangani, Wala mashaka hayachipuki katika nchi;

Ayabu 5:7 Job 5:7

Lakini mwanadamu huzaliwa ili apate mashaka, Kama cheche za moto zirukavyo juu.

Ayabu 5:8 Job 5:8

Lakini mimi ningemtafuta Mungu, Ningemwekea Mungu daawa yangu;

Ayabu 5:9 Job 5:9

Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana; Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu;

Ayabu 5:10 Job 5:10

Yeye atoaye mvua inyeshe juu ya nchi, Na kuyapeleka maji mashambani;

Ayabu 5:11 Job 5:11

Awainuaye juu hao walio chini; Na hao waombolezao hukuzwa wawe salama.

Ayabu 5:12 Job 5:12

Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao.

Ayabu 5:13 Job 5:13

Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka.

Ayabu 5:14 Job 5:14

Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vilevile kama usiku.

Ayabu 5:15 Job 5:15

Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari.

Ayabu 5:16 Job 5:16

Basi hivi huyo maskini ana matumaini, Na uovu hufumba kinywa chake.

Ayabu 5:17 Job 5:17

Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi.

Ayabu 5:18 Job 5:18

Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya.

Ayabu 5:19 Job 5:19

Yeye atakuokoa na mateso sita; Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.

Ayabu 5:20 Job 5:20

Wakati wa njaa atakukomboa na mauti; Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga.

Ayabu 5:21 Job 5:21

Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.

Ayabu 5:22 Job 5:22

Wewe utayacheka maangamizo na njaa; Wala hutawaogopa wanyama wakali wa nchi.

Ayabu 5:23 Job 5:23

Kwani utakuwa na mapatano na mawe ya bara; Nao wanyama wa bara watakuwa na amani kwako.

Ayabu 5:24 Job 5:24

Nawe utajua ya kwamba hema yako ina salama; Na zizi lako utaliaua, wala usikose kitu.

Ayabu 5:25 Job 5:25

Tena utajua ya kwamba uzao wako utakuwa mwingi, Na vizazi vyako watakuwa kama nyasi za nchi.

Ayabu 5:26 Job 5:26

Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.

Ayabu 5:27 Job 5:27

Tazama, haya tumeyapeleleza, ndivyo yalivyo; Yasikie, uyajue, ili upate mema.