Ayabu Mlango 11 Job

Ayabu 11:1 Job 11:1

Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu, na kusema,

Ayabu 11:2 Job 11:2

Je! Huu wingi wa maneno usijibiwe? Na mtu aliyejaa maneno, je! Ahesabiwe kuwa na haki?

Ayabu 11:3 Job 11:3

Je! Majivuno yako yawanyamazishe watu wawe kimya? Nawe hapo ufanyapo dhihaka, je! Hapana mtu atakayekutahayarisha?

Ayabu 11:4 Job 11:4

Kwa kuwa wewe wasema, Mafunzo yangu ni safi, Nami ni safi machoni pako.

Ayabu 11:5 Job 11:5

Lakini, laiti Mungu angenena, Na kuifunua midomo yake juu yako;

Ayabu 11:6 Job 11:6

Tena akuonyeshe hizo siri za hekima, Ya kuwa hufanikiwa katika kuyatimiza makusudi yake! Ujue basi ya kuwa Mungu akuachilia katika uovu wako.

Ayabu 11:7 Job 11:7

Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikilia upeo wa huyo Mwenyezi?

Ayabu 11:8 Job 11:8

Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?

Ayabu 11:9 Job 11:9

Cheo chake ni kirefu kuliko dunia, Ni kipana zaidi ya bahari.

Ayabu 11:10 Job 11:10

Yeye akipita, na kufunga watu, Na kuwaita hukumuni, ni nani basi awezaye kumzuia?

Ayabu 11:11 Job 11:11

Kwani yeye awajua watu baradhuli; Huona na uovu pia, hata asipoufikiri.

Ayabu 11:12 Job 11:12

Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu, Ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda-mwitu.

Ayabu 11:13 Job 11:13

Wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu, Na kumnyoshea mikono yako;

Ayabu 11:14 Job 11:14

Ikiwa una uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe, Wala usikubali upuzi kukaa hemani mwako;

Ayabu 11:15 Job 11:15

Hakika ndipo utakapopata kuinua uso pasipo ila; Naam, utathibitika, wala hutakuwa na hofu;

Ayabu 11:16 Job 11:16

Kwa kuwa utasahau mashaka yako; Utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita;

Ayabu 11:17 Job 11:17

Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri; Lijapokuwa ni giza, litakuwa kama alfajiri.

Ayabu 11:18 Job 11:18

Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini; Naam, utatafuta-tafuta kando yako, na kupumzika katika salama.

Ayabu 11:19 Job 11:19

Tena utalala, wala hapana atakayekutia hofu; Naam, wengi watakutafuta uso wako.

Ayabu 11:20 Job 11:20

Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.