Ayabu Mlango 36 Job

Ayabu 36:1 Job 36:1

Tena Elihu akaendelea na kusema,

Ayabu 36:2 Job 36:2

Ningojee kidogo nami nitakueleza; Kwa kuwa nikali na maneno kwa ajili ya Mungu.

Ayabu 36:3 Job 36:3

Nitayaleta maarifa yangu kutoka mbali, Nami nitampa haki Muumba wangu.

Ayabu 36:4 Job 36:4

Kwani yakini maneno yangu si ya uongo; Aliyekamilika katika maarifa yu pamoja nawe.

Ayabu 36:5 Job 36:5

Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu ye yote; Ana uweza katika nguvu za fahamu.

Ayabu 36:6 Job 36:6

Hauhifadhi uhai wa waovu; Lakini huwapa wateswao haki yao.

Ayabu 36:7 Job 36:7

Yeye hawaondolei macho yake wenye haki; Lakini pamoja na wafalme huwaweka Katika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.

Ayabu 36:8 Job 36:8

Nao wakifungwa kwa pingu, Wakitwaliwa kwa kamba za mateso;

Ayabu 36:9 Job 36:9

Ndipo huwaonyesha matendo yao, Na makosa yao, ya kuwa wametenda kwa kujivuna.

Ayabu 36:10 Job 36:10

Yeye huyafunua masikio yao, wasikie maonyo, Na kuwaagiza warudi kuuacha uovu.

Ayabu 36:11 Job 36:11

Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha.

Ayabu 36:12 Job 36:12

Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga, Nao watakufa pasipo maarifa.

Ayabu 36:13 Job 36:13

Lakini hao wasiomcha Mungu mioyoni hujiwekea hasira Hawalilii msaada hapo awafungapo.

Ayabu 36:14 Job 36:14

Wao hufa wakali vijana, Na uhai wao huangamia katikati ya wachafu.

Ayabu 36:15 Job 36:15

Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake, Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu.

Ayabu 36:16 Job 36:16

Naam, yeye angekuongoza utoke katika msiba Hata mahali penye nafasi, ambapo hapana msonge; Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta.

Ayabu 36:17 Job 36:17

Lakini umejaa hukumu ya waovu; Hukumu na haki hukushika.

Ayabu 36:18 Job 36:18

Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha; Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze.

Ayabu 36:19 Job 36:19

Je! Mali yako yatatosha, hata usiwe katika taabu, Au uwezo wote wa nguvu zako?

Ayabu 36:20 Job 36:20

Usiutamani usiku, Wakati watu wakatwapo katika mahali pao.

Ayabu 36:21 Job 36:21

Jitunze, usiutazame uovu; Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu.

Ayabu 36:22 Job 36:22

Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake; Ni nani afundishaye kama yeye?

Ayabu 36:23 Job 36:23

Ni nani aliyemwagiza njia yake? Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki?

Ayabu 36:24 Job 36:24

Kumbuka kuitukuza kazi yake, Watu waliyoiimbia.

Ayabu 36:25 Job 36:25

Wanadamu wote wameitazama; Watu huiangalia kwa mbali

Ayabu 36:26 Job 36:26

Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; Hesabu ya miaka yake haitafutiki.

Ayabu 36:27 Job 36:27

Kwani yeye huvuta juu matone ya maji, Yamwagikayo katika mvua kutoka kungeni mwake;

Ayabu 36:28 Job 36:28

Ambayo mawingu yainyesha Na kudondoza juu ya wanadamu kwa wingi.

Ayabu 36:29 Job 36:29

Naam, mtu aweza kuelewa na matandazo ya mawingu, Ngurumo za makao yake?

Ayabu 36:30 Job 36:30

Tazama, yeye huutandaza mwanga wake, umzunguke; Naye hufunika vilindi vya bahari.

Ayabu 36:31 Job 36:31

Kwani huwahukumu kabila za watu kwa njia hizi; Hutoa chakula kwa ukarimu.

Ayabu 36:32 Job 36:32

Yeye huifunika mikono yake kwa umeme; Na kuuagiza shabaha utakayopiga.

Ayabu 36:33 Job 36:33

Mshindo wake hutoa habari zake, Anayewaka hasira juu ya uovu.