Ayabu Mlango 26 Job

Ayabu 26:1 Job 26:1

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

Ayabu 26:2 Job 26:2

Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu!

Ayabu 26:3 Job 26:3

Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima! Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi!

Ayabu 26:4 Job 26:4

Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?

Ayabu 26:5 Job 26:5

Hao waliokufa watetema Chini ya maji na hao wayakaao.

Ayabu 26:6 Job 26:6

Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko.

Ayabu 26:7 Job 26:7

Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.

Ayabu 26:8 Job 26:8

Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake.

Ayabu 26:9 Job 26:9

Husitiri uso wa kiti chake cha enzi, Na kulitandaza wingu lake juu yake.

Ayabu 26:10 Job 26:10

Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.

Ayabu 26:11 Job 26:11

Nguzo za mbingu zatetemeka, Na kustaajabu kwa kukemea kwake.

Ayabu 26:12 Job 26:12

Huichafua bahari kwa uwezo wake, Na kumtema Rahabu kwa akili zake.

Ayabu 26:13 Job 26:13

Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake; Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio.

Ayabu 26:14 Job 26:14

Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong'ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuelewa nazo?