Ayabu Mlango 8 Job

Ayabu 8:1 Job 8:1

Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema,

Ayabu 8:2 Job 8:2

Wewe utanena maneno haya hata lini? Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini?

Ayabu 8:3 Job 8:3

Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?

Ayabu 8:4 Job 8:4

Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;

Ayabu 8:5 Job 8:5

Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi;

Ayabu 8:6 Job 8:6

Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.

Ayabu 8:7 Job 8:7

Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.

Ayabu 8:8 Job 8:8

Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;

Ayabu 8:9 Job 8:9

(Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)

Ayabu 8:10 Job 8:10

Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?

Ayabu 8:11 Job 8:11

Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope Na makangaga kumea pasipo maji?

Ayabu 8:12 Job 8:12

Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine.

Ayabu 8:13 Job 8:13

Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;

Ayabu 8:14 Job 8:14

Uthabiti wake utavunjika, Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui.

Ayabu 8:15 Job 8:15

Ataitegemea nyumba yake, isisimame; Atashikamana nayo, isidumu.

Ayabu 8:16 Job 8:16

Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua, Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake.

Ayabu 8:17 Job 8:17

Mizizi yake huzonga-zonga chuguu, Huangalia mahali penye mawe.

Ayabu 8:18 Job 8:18

Lakini, aking'olewa mahali pake, Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona.

Ayabu 8:19 Job 8:19

Tazama, furaha ya njia yake ni hii, Na wengine watachipuka kutoka katika nchi.

Ayabu 8:20 Job 8:20

Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu.

Ayabu 8:21 Job 8:21

Bado atakijaza kinywa chako kicheko, Na midomo yako ataijaza shangwe.

Ayabu 8:22 Job 8:22

Hao wakuchukiao watavikwa aibu; Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena.