Ayabu Mlango 19 Job

Ayabu 19:1 Job 19:1

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

Ayabu 19:2 Job 19:2

Je! Mtanichukiza nafsi yangu hata lini, Na kunivunja-vunja kwa maneno?

Ayabu 19:3 Job 19:3

Mara kumi hizi mmenishutumu; Hamwoni haya kunifanyia mambo magumu.

Ayabu 19:4 Job 19:4

Ingawaje nimekosa, Kosa langu hukaa kwangu mwenyewe.

Ayabu 19:5 Job 19:5

Kwamba mtajitukuza juu yangu, Na kunena juu yangu shutumu langu;

Ayabu 19:6 Job 19:6

Jueni basi kuwa Mungu amenipotosha, Na kunizingira kwa wavu wake.

Ayabu 19:7 Job 19:7

Tazama, nalia, Udhalimu, lakini sisikiwi; Naulilia msaada, wala hapana hukumu.

Ayabu 19:8 Job 19:8

Yeye ameiziba njia yangu nisipate kupita, Na kutia giza katika mapito yangu.

Ayabu 19:9 Job 19:9

Amenivua utukufu wangu, Na kuiondoa taji kichwani mwangu.

Ayabu 19:10 Job 19:10

Amenibomoa pande zote, nami nimetoweka; Na tumaini langu ameling'oa kama mti.

Ayabu 19:11 Job 19:11

Tena ameziwasha ghadhabu zake juu yangu, Akanihesabia kuwa mmoja katika watesi wake.

Ayabu 19:12 Job 19:12

Majeshi yake husongea pamoja, na kunipandishia njia yao, Na kupiga marago kuizunguka hema yangu.

Ayabu 19:13 Job 19:13

Amewaweka ndugu zangu mbali nami, Na wanijuao wametengwa nami kabisa.

Ayabu 19:14 Job 19:14

Watu wa mbari yangu wamekoma, Na rafiki zangu niwapendao wamenisahau.

Ayabu 19:15 Job 19:15

Wakaao nyumbani mwangu, na vijakazi vyangu, wanihesabu kuwa mgeni; Mimi ni mgeni machoni pao.

Ayabu 19:16 Job 19:16

Namwita mtumishi wangu, wala haniitikii, Ingawa namsihi kwa kinywa changu.

Ayabu 19:17 Job 19:17

Pumzi zangu ni kama za mgeni kwa mke wangu, Nami ni machukizo kwa ndugu zangu.

Ayabu 19:18 Job 19:18

Hata watoto wadogo hunidharau; Nikiondoka, huninena.

Ayabu 19:19 Job 19:19

Wasiri wangu wote wanichukia; Na hao niliowapenda wamenigeukia.

Ayabu 19:20 Job 19:20

Mfupa wangu unagandamana na ngozi yangu na nyama yangu, Nami nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu.

Ayabu 19:21 Job 19:21

Nihurumieni, nihurumieni, enyi rafiki zangu, Kwa maana mkono wa Mungu umenigusa.

Ayabu 19:22 Job 19:22

Mbona ninyi mnaniudhi kama Mungu, Wala hamkutosheka na nyama yangu?

Ayabu 19:23 Job 19:23

Laiti maneno yangu yangeandikwa sasa! Laiti yangeandikwa kitabuni!

Ayabu 19:24 Job 19:24

Yakachorwa katika mwamba milele, Kwa kalamu ya chuma na risasi.

Ayabu 19:25 Job 19:25

Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.

Ayabu 19:26 Job 19:26

Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;

Ayabu 19:27 Job 19:27

Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu.

Ayabu 19:28 Job 19:28

Kama mkisema, Jinsi tutakavyomwudhi! Kwa kuwa shina la jambo hili limeonekana kwake;

Ayabu 19:29 Job 19:29

Uogopeni upanga; Kwa maana adhabu za upanga zina ghadhabu, Mpate kujua ya kwamba hukumu iko.