Ayabu Mlango 15 Job

Ayabu 15:1 Job 15:1

Ndipo Elifazi, Mtemani, akajibu, na kusema,

Ayabu 15:2 Job 15:2

Je! Yapasa mtu mwenye hekima kujibu kwa ujuzi wa uvuvio, Na kujaza tumbo lake na upepo wa mashariki?

Ayabu 15:3 Job 15:3

Je! Ahoji na mazungumzo yasiyo faida, Au kwa maneno ambayo hawezi kufanya mema kwayo?

Ayabu 15:4 Job 15:4

Naam, wewe waondoa kicho, Nawe wazuia ibada mbele za Mungu.

Ayabu 15:5 Job 15:5

Kwani uovu wako unakufundisha kinywa chako, Nawe wachagua ulimi wake mwenye hila.

Ayabu 15:6 Job 15:6

Kinywa chako mwenyewe chakuhukumia makosa, wala si mimi; Naam, midomo yako mwenyewe hushuhudia juu yako.

Ayabu 15:7 Job 15:7

Je! Wewe u mtu wa kwanza aliyezaliwa? Au, ulizawa wewe kabla ya milima?

Ayabu 15:8 Job 15:8

Je! Umesikia mashauri ya siri ya Mungu? Nawe je! Wazuia hekima iwe yako tu?

Ayabu 15:9 Job 15:9

Je! Wewe wajua neno lipi, ambalo sisi hatulijui? Nawe wafahamu nini, ambalo halimo ndani yetu?

Ayabu 15:10 Job 15:10

Wenye mvi, na walio wazee sana, wote wapo pamoja nasi, Ambao ni wazee kuliko baba yako.

Ayabu 15:11 Job 15:11

Je! Utulizi wa Mungu ni mdogo sana kwako, Na hilo neno la upole si kitu kwako?

Ayabu 15:12 Job 15:12

Mbona moyo wako unakutaharakisha! Na macho yako, je! Kwani kung'ariza?

Ayabu 15:13 Job 15:13

Hata ukageuza roho yako iwe kinyume cha Mungu, Na kuyatoa maneno kama hayo kinywani mwako.

Ayabu 15:14 Job 15:14

Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?

Ayabu 15:15 Job 15:15

Yeye hawategemei watakatifu wake; Naam, mbingu nazo si safi machoni pake.

Ayabu 15:16 Job 15:16

Sembuse mtu ambaye ni mwenye kuchukiza na uchafu, Mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji!

Ayabu 15:17 Job 15:17

Mimi nitakuonyesha, unisikilize; Na hayo yote niliyoyaona nitayanena;

Ayabu 15:18 Job 15:18

(Ambayo watu wenye hekima wameyatangaza Tokea baba zao, wala hawakuyaficha;

Ayabu 15:19 Job 15:19

Waliopewa hiyo nchi peke yao, Wala mgeni hakupita kati yao);

Ayabu 15:20 Job 15:20

Mtu mwovu huwa na uchungu siku zake zote, Hata hesabu ya miaka aliyowekewa mwenye kuonea.

Ayabu 15:21 Job 15:21

Sauti za utisho zi masikioni mwake; Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;

Ayabu 15:22 Job 15:22

Yeye hasadiki kwamba atarudi kutoka gizani, Naye hungojewa na upanga;

Ayabu 15:23 Job 15:23

Hutanga-tanga ili apate chakula, akisema, Ki wapi? Ajua kwamba siku ya giza i tayari karibu yake;

Ayabu 15:24 Job 15:24

Mateso na dhiki humtia hofu; Humshinda kama vile mfalme aliye tayari kwa vita;

Ayabu 15:25 Job 15:25

Kwa kuwa amenyosha mkono wake juu ya Mungu, Na kuendelea kwa kiburi kinyume cha Mwenyezi;

Ayabu 15:26 Job 15:26

Humshambulia na shingo ngumu, Kwa mafundo makubwa ya ngao zake;

Ayabu 15:27 Job 15:27

Kwa kuwa amefunika uso wake na kunona kwake, Na kuwandisha mafuta kiunoni mwake; Naye amekaa katika miji iliyo ukiwa,

Ayabu 15:28 Job 15:28

Katika nyumba ambazo hapana mtu azikaaye, Zilizokuwa tayari kuwa magofu.

Ayabu 15:29 Job 15:29

Hatakuwa tajiri, wala mali zake hazitadumu, Wala maongeo yao hayatainama nchi.

Ayabu 15:30 Job 15:30

Hataondoka gizani; Ndimi za moto zitayakausha matawi yake, Naye ataondoka kwa pumzi za kinywa chake.

Ayabu 15:31 Job 15:31

Asiutumainie ubatili, na kujidanganya; Kwa kuwa huo ubatili ndio utakaokuwa ujira wake.

Ayabu 15:32 Job 15:32

Jambo hili litatendeka kabla ya wakati wake, Na tawi lake halitasitawi.

Ayabu 15:33 Job 15:33

Atayapukutisha mapooza yake kama mzabibu, Na kuyatupa maua yake kama mzeituni.

Ayabu 15:34 Job 15:34

Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.

Ayabu 15:35 Job 15:35

Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu, Nalo tumbo lao hutengeza udanganyifu.